TAKUKURU yaagizwa kuchunguza Ufisadi Skimu ya Umwagiliaji Mombo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku
Gallawa ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
kumchunguza Afisa Kilimo wa Wilaya ya Korogwe Bw. Rugembe Kakuru kutokana na utata
wa matumizi ya zaidi ya shiling million 200 za Skimu ya mpunga ya Mombo.
Mradi wa umwagiliaji Skimu ya
Mombo ilipata zaidi ya shilingi million 200 tangu January mwaka jana na
licha ya kuwepo kwa fedha hizo mpaka sasa hakuna kilichofanyika jambo linalotia
shaka.
Mhe. Gallawa aliitaka taasisi hiyo
kumchunguza Afisa huyo kuhusiana na mazingira ya uendeshaji wa zoezi la
ukarabati wa mfereji wa skimu hiyo pamoja na kufanya michoro kwa shilingi
Milioni 100 jambo alilolieleza kuwa ni ufisadi wa mali ya Umma.
“Bwana takukuru hebu niambie kufanya
Cotetion kwa shilingi milion 100 wewe inakuingia kichwani kweli……huyu bwana (Afisa
kilimo Wilaya) muwe naye aeleze vizuri, ama tumshughulikie wenyewe” alisema
Mhe. Gallawa wakati akimkabidhi Afisa huyo mikononi mwa taasisi hiyo.
Mhe.Gallawa ambaye alikuwa katika
ziara ya siku tano kukagua miradi na kuhamasisha shughuli za maendeleo Wilayani Korogwe alieleza
kuwa haoni sababu za msingi zilizofanya ukarabati wa mfereji wa mradi huo
kusimama wakati fedha zilishaingizwa na kudai kuwa huo ni uzembe na njama za
wataalamu kudhoofisha juhudi za serikali na wananchi.
Hata
hivyo akizungumza katika mkutano na wanaushirika wa mradi huo Mhe. Gallawa alitumia nafasi hiyo kuwataka
wananchi kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa za viongozi wenye tabiaza kukwamisha maendeleo ikiwemo ufujaji wa mali za Umma ili
kuwezesha kuchukuliwa hatua kabla hawajaleta hasara kubwa.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Korogwe Bw. Rugembe
Kakuru akitolea ufafanuzi utata wa matumizi ya millioni 200 ya skimu ya Mpunga
ya Mombo kwa Mkuu wa Mkoa Mhe.Chiku Gallawa
Meneja wa Skimu ya Umwagiliaji ya
Mombo Bw. Mwenda akielezea maendeleo ya Skimu hiyo kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Gallawa
0 comments: