Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa viwanja vya Uhuru Park Tanga Leo
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego akiweka Ngao na Mkuki
kwenye mnara wa Mashujaa wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa iliyofanyika kwenye viwanja vya Uhuru Park Jijini Tanga leo. Tarehe
25 Julai ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa
wa Tanzania waliopigana vita na
maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka. Mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika Mkoa wa
Kagera Wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya Mashujaa yaliyopo Kaboya
Base
commander Mkoa wa Tanga Kanali L.
Mwakibinga akiweka Sime kwenye mnara wa Mashujaa
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Constatine Massawe akiweka Shada la Maua
kwenye mnara wa mashujaa
Meya
wa Jiji la Tanga Mhe. Omari Guledi
akiweka Upinde na Mshale kwenye mnara wa mashujaa
Askari
mstaafu aliyepigana vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1939- 1947 Bw.Francis Benado akielekea
mnara wa mashujaa kuweka Shoka.
Akizungumza baada ya maadhimisho ameisihi jamii kumrudia Mungu ili roho kuwa
safi na kufanya kazi bila kuwa na uroho wa madaraka na kuweka tamaa nyuma
akimtolea mfano Baba wa Taifa Mwl. Julias Kambarage Nyerere
Muonekano wa Mnara wa Mashujaa Jijini
Tanga leo baada ya kumaliza kuweka siraha mbalimbali
Askari Mgambo wakiwa kwenye gwaride wakati wa
maadhimisho
Baadhi ya wakazi wa Tanga wakiwa kwenye maadhimisho hayo
0 comments: