Mkuu wa Mkoa wa Tanga Agiza Maafisa Mipango Kuwashirikisha Wananchi katika Mipango ya Maendeleo
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe.Chiku Gallawa akizungumza na Maafisa Mipango wa
Halmashauri za Mkoa wa Tanga(hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi
ya Mkoa, kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw.Benedict Ole Kuyan.
Baadhi
ya Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye Ukumbi wa
Mikutano Ofisi ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Chiku Gallawa ameagiza Maafisa Mipango kuwashirikisha wananchi katika kuleta
maendeleo na kuwataka watoke Maofisini waende Vijijini kukutana na waalengwa na kuacha kutumia mawazo
ya Watendaji, wito huo aliutoa kwenye kikao kilicho husisha Maafisa Mipango wa
Halmashauri za Mkoa wa Tanga kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya
Mkoa mwishoni mwa wiki.
Maafisa Mipango wafikirie
vipaumbele vya Maendeleo kwa wananchi katika eneo husika ili kujua changamoto
zinazowakabiri kwa kuitisha mikutano ya hadhara kila baada ya Miezi Mitatu na pia amewataka Maafisa Mipango kubuni vyanzo vya mapato kuliko kutegemea pesa kutoka
Serikalini.
Mhe. Gallawa amesisitiza kuwa Wananchi wanatakiwa wawe watu wa naoibua mipango wakihusishwa kuanzia ngazi
ya Kijiji hadi Halmashauri na sio watendaji wa Vijiji na Kata ambao hutumia
zaidi Mawazo yao ambayo hupelekea Mipango duni kwa Serikali.
Katika Mpango wa Mabadiliko Makubwa Sasa(BRN) Mhe.
Gallawa alitaja vipaumbele vya Mkoa wa Tanga kuwa ni Mapato, Huduma za Jamii na
Mazingira.Kwa upande wa Mapato amesisitiza Pato la Mtu binafsi kwa kuanzisha
mfumo utakao mwezesha mzalishaji wa kwaida ambao utajumuisha Masoko na
Usafirishaji kwa kutumia Stakabadhi.
0 comments: