Kamati Ya Bunge ya LAAC Yapongeza Utekelezaji Miradi Korogwe Mji
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) inayoendelea na ziara yake mkoani Tanga
imepongeza utekelezaji wa miradi tisa ya maendeleo waliyoikagua katika
halmashauri ya Korogwe mji na kusema inaonesha thamani halisi ya fedha.
Miradi hiyo ya maendeleo ikiwemo
iliyokaguliwa na kamati hiyo ni ile iliyopita fedha ya ruzuku ya serikali ya
jumla ya sh. 2,109,298.95 ambayo ilipitishwa na Bunge katika bajeti ya mwaka wa
fedha wa 2011/2012.
Hayo yamebainishwa wakati wa
ziara ya wajumbe wa kamati hiyo mjini Korogwe.
Miradi hiyo imejumuisha ujenzi wa
vyumba vya madarasa, ukarabati wa skimu ya umwagiliaji maji Kwamngumi, kuchimba
visima vya maji Kwakombo na Kwameta na ujenzi wa Maabra.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
mara baada ya ukaguzi wa miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Rajabu Mbarouk
alisema utekelezaji wa miradi hiyo waliyoitembelea umewapa faraja kutokana na
uhalisia wake.
“Miradi yote kwa kweli imetuvutia
sana kila kitu ikiwemo mikataba, taratibu za manunuzi na mambo yote muhimu
yamezingatiwa na jambo zuri zaidi ni kuonekana kwa thamani halisi ya
fedha hizo za umma ki msingi tunawapongeza sana watendaji hawa”, alisema.
Stori na Anna Makange- Habari Leo
0 comments: