Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Kitaifa yafanyika Wilayani Korogwe Mkoani Tanga

 


     Siku ya wazee duniani imefanyika kitaifa Wilayani Korogwe  Mkoani Tanga na kuhudhuriwa na mamia ya wazee na wananchi kwa ujumla. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mhe. Dk Mohamed G. Bilali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja na mgeni rasmi pia viongozi mbalimbali wa kiserikali wa ngazi ya kitaifa na kimkoa wamefika katika maadhimisho hayo akiwemo Mhe. Aggrey Mwanri, Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI, Mhe. Seif S.Rashid, Naibu Waziri wa Afya, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wakuu wa Wilaya za Tanga, Wabunge, Viongozi wa CCM, Viongozi wa dini na viongozi wa vyama  mbalimbali vya siasa.

Siku ya wazee duniani huadhimishwa kila tarehe mosi mwezi wa Octoba ikiwa ni siku iliyotengwa rasmi kwa ajili ya kutafakari mahitaji  na umuhimu wa wazee katika jamii. Kauli mbiu ya siku ya wazee mwaka huu nchini ni “Matarajio ya wazee ni heshima, usalama na maisha mema” Nayo Serikali imewahakikishia wazee maisha mema na imeahidi kuzimamia zoezi la upatikanaji wa huduma za afya bure bila usumbufu.

 

  Mhe. Chiku Gallawa Mkuu wa Mkoa wa Tanga akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Bilali mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kubariki  maadhimisho ya siku ya wazee duniani  ambayo yanafanyika Korogwe

Serikali inatambua umuhimu wa wazee katika jamii bila ya kujali rangi, kabila wala itikadi za dini. Mhe. Bilal akisalimiana na Mzee ambaye ni kada wa Chadema

 Maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa Korogwe  yamepambwa na mvua kubwa lakini wazee hawakuwa nyuma kusherekea siku yao hii muhimu. Pichani ni maandamano ya wazee kuelekea uwanja wa sherehe

Mzee Clement Nsherenguzi  mwenye umri wa miaka 77 ambaye  ni mwandishi wa radio Fadeko na radio Karagwe  akiwa kazini kuchukua matukio. Mzee huyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Saidia Wazee anaungana na wazee wengine nchini kuiomba serikali kuendelea kupigani maslahi ya wazee

Ulifika muda wa wazee kuburudika na vikundi mbalimbali vilipamba maadhimisho hayo

Baadhi ya wazee na wananchi wa kawaida waliofika Korogwe katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani

 
 
 Wazee wamepata fursa ya kupima afya zao kwa magonjwa yasiyoambukizi. Pichani ni mzee akipima uzito na presha



Written by

0 comments: