Maafisa Elimu wasisitiziwa Uwajibikaji ili kupandisha Ufaulu Mkoani Tanga



Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa amewasisitiza Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari wa Mkoa wa Tanga kufanya kazi kwa juhudi na weledi ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi. Hayo ameyasema wakati wa kikao cha Maafisa Elimu kilichofanyika Wilayani Korogwe kutathmini mikakati ya kila Halmashauri iliyojipangia ikiwa ni msingi wa Utekelezaji wa mkakati wa Matokeo Makubwa (Big Results Now) wa Taifa.

Aidha Maafisa hao waliagizwa kuachia ngazi kwa kuandika barua ya kuacha kazi kwa hiari kama wanahisi hawako tayari kwenda na kasi ya Mkakati wa Taifa wa “Big Results Now” ili nguvu kazi iliyo na uwezo iweze kuchukua nafasi hizo. Lengo kuu ni kupandisha kiwango cha ufaulu  kutoka asilimia 45 hadi 75  katika mitihani ya Kifaifa ya msingi na Sekondari .

Akionyesha msisitizo, Mhe. Gallawa amezitaka Halmashauri kuhakikisha zinatekeleza malengo hayo ya ufaulu kwa watahiniwa wa mitihani ya kifaifa itakayofanyika mwaka huu 2013 ukianzia na darasa la saba  na kidato cha nne.

Akionyesha kutoridhishwa na taarifa za mikakati zilizoandaliwa na Halmashauri hizo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmahauri kujiwekea mikakati inayotekelezeka kwani matokea yake ni mazuri  badala ya ile ambayo ni nadharia tu na haiwezi kuwanufaisha wananchi.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan amewasisitiza Maafisa Elimu kuachana na dhana ya kufanya kazi kwa mazoea bali kuwajibika zaidi  ili kuleta matokeo mazuri ya ufaulu katika Mkoa wa Tanga.

Wakibainisha sababu za ufaulu mdogo wa   wanafunzi  hasa wa darasa la saba  kwa mwaka  2012, Maafisa Elimu wamesema  Form za OMR zilikuwa  changamoto  kwa wanafunzi hivyo kuahidi kutoa elimu ya jinsi ya kuzitumia kabla ya kufanya mitihani ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini wakati wa kujijaza.
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Chomola  ( kulia) , RPC Constantine Massawe  (wa pili kulia) na  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan (wa tatu kulia)
wakilisiliza kwa makini.
Baadhi ya Maafisa Elimu wa Shule za Msingi na Sekondari  na Wakurugenzi wa Halmashauri waliohudhuria Kikao hicho


Written by

2 comments:

  1. Good start!use proper words,avoid the use of abbreviations and do proof reading b4 publishing

    ReplyDelete
  2. nice beginning, congrats Tanga region, let it be on-going mission perhaps we shall witness changes

    ReplyDelete