BREAKING NEWS
AJALI YA JAHAZI MV MUNA
Watu 12
wamenusurika kufa baada ya jahazi la mizigo liitwalo MV Muna lenye namba za
usajili T.0083 liliyokuwa na mizigo kiasi cha tani 50 likitokea nchini Kenya kwenda Visiwani Zanzibar kuzama
katika eneo la Kigombe Wilayani Muheza
usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe amethibitisha kutokea tukio hilo na
kueleza kuwa kuzama kwa jahazi kulitokana na mashine zake kugoma na kuanza
kuzama.
Abiria
waliosalimika wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bombo Mkoani Tanga kwa ajili ya
kuchunguzwa afya zao kutokana na dhoruba walikuwa wameipata wakati Jahazi hilo
lilipokuwa limezama.
0 comments: