“RETREAT” YA UONGOZI WA KIMKAKATI KWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO YALENGA MABADILIKO YA UTENDAJI KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA TANGA NA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO.





Bw: Benedict Ole Kuyan, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga akitoa maada maalumu juu ya uongozi wa kimkakati  wakati wa “RETREAT” ya watumishi ambao ni wakuu wa wa Idara na Vitengo iliyofanyika kwa muda wa siku mbili wilayani Pangani . Lengo kuu lilikuwa ni kuwaleta wakuu hao pamoja ili kupata elimu zaidi juu ya kufanya madiliko ya kuboresha utendaji katika idara na vitengo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga na Hospitali ya Rufaa ya Bombo.



Washiriki waligawanyika kwenye makundi mawili na kujadili jinsi ya kuimarisha utendaji mzuri katika maeneo ya mawasiliano na ukaguzi.




Washiriki wa “RETREAT” walipata fursa ya chemsha bongo. Kila mmoja alihitajika kujitathimini utendaji wake kwa kujaza form maalumu ambayo ililenga kusaidia kujua uweledi na udhaifu wa kila mmoja ili kutafuta namna ya kujirekebisha.

Washiriki wa “RETREAT” wakisikiliza mojawapo ya maada zilizotolewa  kwa makini.


Picha ya pamoja  ya KatibuTawala Mkoa wa Tanga  ( wa nne kulia) pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga na Hospitali ya Rufaa ya  Bombo.


Written by

0 comments: