Matangazo ya Kituo cha Televisheni cha Halmashauri , Tanga Televisheni Yarejeshwa Rasmi



Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Omari Guledi  Mohamed akiongea wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari  ofisini kwake leo juu ya urejeshwaji rasmi wa matangazo ya kituo cha Televisheni cha Tanga Televisheni kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga. Matangazoyameanza Juni 12 , 2014 kituo kilipoanza kurusha matangazo ya majaribio. 
 
Matangazo hayo yanapatikana kupitia king’amuzi cha kampuni ya Startimes, channel no 109 katika Mkoa wa Tanga. Kituo cha Tanga Televisheni kilikatisha matangazo yake mnamo tarehe 12 Januari, 2013 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utangazaji ambapo awali kiliendeshwa kwa mfumo wa analogia.

Kwa sasa kituo cha Tanga TV kinaonekana  katika maeneo ya Wilaya za Tanga, Muheza, Pangani, Mkinga na Pemba  ambapo Uongozi wa Halmashauri unafanya jitihada zaidi ili kuwafikia wakazi wote wa Wilaya za Tanga. Tanga Televisheni ni kituo cha kwanza cha Halmashauri nchini kuingia katika mfumo wa digitali.

            Wito unatolewa kwa Wakazi wa Tanga  kukipenda na kutumia kituo hiki kupata   
           taarifa    mbalimbali za mkoa wa Tanga na kitaifa na pia katika kukuza vipaji vyao 
           kupitia kazi za kitaaluma, michezo na pia  kazi za sanaa.
 Kulia ni Bw. Musa Labani, Mkuu wa Kituo cha Tanga Televisheni  pamoja na Wanahabari kutoka Kituo hicho
 Waandishi wa Habari wa Tanga wakati wa mkutano


Written by

0 comments: