Dc Handeni Ameagiza Wanasiasa Wanaozuia Wananchi Kuchangia Ujenzi Wa Maabara Wakamatwe


Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Muhingo Rweymamu ameagiza wanasiasa wanaozuia wananchi kuchangia ujenzi wamakatwe pamoja na kuchukuliwa hatua kali kwa sababu wanachangia kurudisha nyuma maendeleo katika Wilaya.
                                
Agizo hilo limetolewa juzi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara katika shule mbalimbali wilayani Handeni.

Akiwa kwenye shule ya sekondari ya sekondari Mkata aligundua ujenzi huo kuendelea kwa kuasuasua kutokana na wananchi wengi kushindwa kuchangia kikamilifu kunakosababishwa na baadhi ya wanasiasa kuwazuia kuachakufanyahivyo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa masuala ya siasa hayawezi kuingiliana na sekta ya elimu hiyo viongozi wa vyama hivyo watakaobainika kushiriki kwa namna moja au nyengine kuzuia ujenzi huu wakamatwe wapelekwe kwenye vyombo vya kisheria.

   “Mimi nasema hivi kama kuna wanasiasa wanachangia kuzorotesha michango ya ujenzi wa maabara hii hatuweza kuivumilia lazima tuwashughulikie hata kama wakiwa ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) “AlisemaMuhingo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Handeni (CCM), Athumani Malunda alisema kuwa chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa maabara lakini vyama vyingine vimekuwa vikiwashawishi wananchi kuacha kufanya hivyo.

Aidha aliwataka watendaji kupewa ridhaa ya kuwakamatwa viongozi wa vyama vya siasa ambao wanahamasisha wananchi kuacha kuchangia maendeleo ya ujenzi wa maabara wakamatwe pamoja na kufikishwa mahakamani.

   “Nadhani kuwepo kwa sheria kali za kuchukuliwa kwa wanasiasa wanaowashawishi wananchi kuacha kuchangia ujenzi wa maabara kwa sababu wakiendelea kuachiwa kufanya hivyo watarudisha nyuma maendeleo yetu “Alisema Malunda ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni.

Katika hatua nyengine,DC Muhingo aliwataka wananchi pamoja na watendaji wa ngazi za chini kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kuweza kuharakisha kasi ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Muhingo Rweymamu kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Sindeni.Picha & stori na Osca Assenga Handeni.


Written by

0 comments: