Uzinduzi Wa Kuhamasisha Wananchi Kujiunga Na Mfuko Wa Afya Ya Jamii(CHF) Wilaya ya Muheza, Zaidi Ya Kaya 65 Zajiunga hapo kwa papo

 Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Subira Mgalu akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya  Potwe wilayani Muheza uliofanyika  leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga hapo kwa papo

 Mmoja wa  Maafisa kutoka  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) akihamashaa kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi



Afisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)kutoka Makao  Makuu Isaya Shekifu wa pili kulia akifuatilia uandikishwaji wa wanachama wapya wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) leo (Jana) wakati wa uzinduzi wake uliofanyika Kata ya Potwe Wilayani Muheza wa kwanza kulia ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe kulikofanyika uzinduzi huo,Dr.Swalehe Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza  wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) Picha & stori na Osca Assenga- Muheza


Written by

0 comments: