RHMT Tanga yajikita katika uboreshaji wa huduma za afya



 
Timu ya Uendeshaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Tanga (RHMT) imeendelea kuhakikisha kuwa huduma za Afya katika Vituo mbalimbali vya afya katika Mkoa wa Tanga zinakuwa na mazingira mazuri ya kuviwezesha kutoa huduma bora.
Hayo yanathibitishwa na usimamizi unaofanywa mara kwa mara na timu ya Usimamizi wa huduma za afya ya  Mkoa. Lengo kuu ni kutaka kujua mazingira ya kazi na changamoto zinazojitokeza katika vituo vya afya katika Mkoa wa Tanga na hatimaye kuona ni jinsi gani mamlaka za Mkoa zinavyoweza kuboresha huduma.
Ikiwa kwenye usimamizi shirikishi katika Wilaya ya Mkinga wiki iliyopita, timu ya Mkoa iliyokuwa na wajumbe watano ambayo wajumbe wake ni  Dr  Clemence Marcel, Neema Shosho, Charles Kijazi , Monica Laurent na  Joyce Magembe  iliweza kujionea hali halisi ya mazingira ya kazi katika vituo mbalimbali vya afya  na kubaini kuwa ipo changamoto ya wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya  (CHF).  
Ilionekana pia  kuwa ipo haja ya viongozi wa serikali  na viongozi wakisiasa  kuwa mstari wa mbele katika kuwahamaisha wananchi ili kujiunga na mfuko huu muhimu. Faida zinazotokana na Bima ya afya (CHF) ni pamoja na faida ya tele kwa tele ambayo kituo cha afya hupatiwa kutokana  na uchangiaji wa wananchi katika kituo husika.
Timu pia iliweza kupata  fursa ya  kutoa ushauri kwa ngazi mbalimbali za Wilaya ili kusaidia  upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwa wakati.
 
Dr Justice Munisi ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkinga akielezea mpango kazi wa idara ya Afya katika Wilaya yake  wakati timu ya RHMT ilipofika ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya usimamizi shirikishi katika Wilaya ya Tanga . Kulia ni timu ya usimamizi huduma za afya katika Wilaya ya Mkinga wakifuatilia kwa makini.
 Dr Amina S. Ally ambaye ni Mtabibu katika kituo cha afya cha Mayomboni  akitoa taarifa ya utendaji kwa timu ya utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo. Kulia ni Charles Kijazi, Neema Shosho (Katikati ) na Dr Clemence Marcel
Bi. Pili Azizi (kushoto) ambaye ni Mtabibu Msaidizi katika kituo cha afya cha Moa  akionyesha sehemu ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba kwa timu ya utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo. kulia ni Dr Clemence Marcel na Charles Kijazi
Dr.Mohamed Ally  ambaye ni Mtabibu katika Kituo cha afya cha  Vyeru  akifafanua jambo kwa timu ya utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo
 
 



Written by

0 comments: