Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga Azindua Mpango Mkakati Wa Miaka Mitano Wa Ukimwi Katika Mkoa Wa Tanga Wakati Wa Kikao Cha RCC
Mhe.
Magalula Said Magalula , Mkuu wa Mkoa wa Tanga akikata utepe uliofungwa kwenye
kitabu kuashiria uzinduzi wa Mpango wa
Miaka mitano wa Ukimwi katika Mkoa wa Tanga wakati wa kikao cha Ushauri cha
Mkoa wa Tanga (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki.
Mada
mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa katika kikao hicho zikiwemo mada juu ya Taarifa ya upatikananji
maji katika Mkoa wa Tanga, taarifa ya Bima ya Afya, taarifa ya hali ya bandari
ya Tanga, taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya 2014/2015 na mapenekezo ya bajeti
ya mwaka 2015/2016.
Wajumbe
walipata nafasi ya kujadiliana jinsi ya kuboresha huduma na vilevile mikakati
juu ya kukabiliana na baadhi ya changamoto. Naye Mkuu wa mkoa ambaye alikuwa
Mwenyekiti wa kikao alitoa maelekezo juu ya nini kifanyike ili huduma za
wananchi ziweze kuboreshwa.
Baadhi
ya Wajumbe na waalikwa wakisikiliza mijadala mbalimbali
Baadhi
ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
0 comments: