Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) Umezindua Rasmi Zoezi La Utambuzi Na Usajili Wa Watu Katika Mkoa Wa Tanga
Joseph Makani, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) akizungumza wakati wa uzinduzi. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa , Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw.Salum Mohamed
Chima (Alhaj) na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Halima Dendego
WAKUU wa Wilaya,
Wakurugenzi, Watendaji katika ngazi zote Tarafa, Kata, Mitaa, Vijiji na
Vitongoji, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya Siasa wameagizwa kuonyesha
ushirikiano katika kuhakikisha jukumu la
utambuzi na usajili wa watu linaenda sawasawa na maagizo ya Serikali .
Msisitizo huo umetolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ambaye ameahidi kutoa ushirikiano
wakati akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu uliofanyika mapema
leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho( NIDA) Bw. Joseph Makani amewataka wakazi wa Tanga
kujitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi zima kwani zoezi hilo Mkoani Tanga ni utekelezaji wa Mpango wa
Usajili wa Wakazi waishio Kihalali Nchini kwa lengo la kuwapatia vitambulisho
vya Taifa kwa hadhi ya raia, Wageni wakazi na Wakimbizi.
“Fichueni wale ambao
hawastahili kupata vitambulisho vya uraia kwa kutoa taarifa katika ofisi za
uhamiaji na polisi ili taifa lisije likaingia katika hatari ya kuwasajili
wageni kama raia”amesisitiza Makani.
Zoezi la Utambuzi na Usajili Mkoani Tanga
linategemea kuanza Oktoba 12 mwaka huu. Wananchi wanaombwa kuhakikisha
wanajisajili kwa wenyeviti wa mitaa ili kurahisisha zoezi hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akizindua rasmi zoezi la utambuzi na
usajili wa watu
Katibu
Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima ( Alhaji) akizunguza muda mchache
kabla ya uzinduzi
Baadhi ya viongozi wawakilishi kutoka katika Wilaya za
Tanga wakati wa uzinduzi
Mimi shabiri Hemedi Bakari mzaliwa wa Tanga, jina langu la la NIDA limekisewa, nataka kurekebisha ila sijui niende wapi
ReplyDelete