Maafisa Elimu wasisitiziwa Uwajibikaji ili kupandisha Ufaulu Mkoani Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Chiku Gallawa amewasisitiza Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari wa Mkoa wa
Tanga kufanya kazi kwa juhudi na weledi ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi.
Hayo ameyasema wakati wa kikao cha Maafisa Elimu kilichofanyika Wilayani
Korogwe kutathmini mikakati ya kila Halmashauri iliyojipangia ikiwa ni msingi
wa Utekelezaji wa mkakati wa Matokeo Makubwa (Big Results Now) wa Taifa.
Aidha Maafisa hao
waliagizwa kuachia ngazi kwa kuandika barua ya kuacha kazi kwa hiari kama
wanahisi hawako tayari kwenda na kasi ya Mkakati wa Taifa wa “Big Results Now” ili nguvu kazi iliyo na
uwezo iweze kuchukua nafasi hizo. Lengo kuu ni kupandisha kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 45 hadi 75 katika mitihani ya Kifaifa ya msingi na
Sekondari .
Akionyesha msisitizo, Mhe.
Gallawa amezitaka Halmashauri kuhakikisha zinatekeleza malengo hayo ya ufaulu
kwa watahiniwa wa mitihani ya kifaifa itakayofanyika mwaka huu 2013 ukianzia na
darasa la saba na kidato cha nne.
Akionyesha kutoridhishwa
na taarifa za mikakati zilizoandaliwa na Halmashauri hizo, Mhe. Mkuu wa Mkoa
amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmahauri kujiwekea mikakati
inayotekelezeka kwani matokea yake ni mazuri
badala ya ile ambayo ni nadharia tu na haiwezi kuwanufaisha wananchi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa
wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan amewasisitiza Maafisa Elimu kuachana na dhana
ya kufanya kazi kwa mazoea bali kuwajibika zaidi ili kuleta matokeo mazuri ya ufaulu katika
Mkoa wa Tanga.
Wakibainisha sababu za
ufaulu mdogo wa wanafunzi hasa wa darasa la saba kwa mwaka 2012, Maafisa Elimu wamesema Form za OMR zilikuwa changamoto
kwa wanafunzi hivyo kuahidi kutoa elimu ya jinsi ya kuzitumia kabla ya
kufanya mitihani ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini wakati wa
kujijaza.
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Chomola ( kulia) , RPC Constantine Massawe (wa pili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan (wa tatu kulia)
wakilisiliza kwa makini.
Baadhi ya Maafisa Elimu wa Shule za Msingi na
Sekondari na Wakurugenzi wa Halmashauri waliohudhuria
Kikao hicho
Good start!use proper words,avoid the use of abbreviations and do proof reading b4 publishing
ReplyDeletenice beginning, congrats Tanga region, let it be on-going mission perhaps we shall witness changes
ReplyDelete