Mbuga ya Saadani, Hifadhi yenye vitu ambavyo havipatikani katika Mbuga nyingine
Japo
si maarufu miongoni mwa wengi lakini Saadani ni hifadhi ya kipekee yenye
vivutio vizuri vya kitalii vinavyoweza kulitangaza taifa na kuongeza pato lake.
Mbuga
ya Saadani ni miongoni mwa hifadhi 16 za taifa. Hifadhi hii iko chini ya
Mamlaka za Hifadhi za Taifa (Tanapa) ilianzishwa mwaka 1962 ikiwa ni pori la
akiba. Baadaye mwaka 2005, ilipandishwa hadhi rasmi na kuwa hifadhi ya taifa.
Mbuga hii ipo Mikoa ya Pwani na Tanga, kwa upande wa
Kaskazini ipo Wilayani Pangani , Bagamoyo (kaskazini) na
Zanzibar.
Kutoka Jiji la Tanga kuna umbali wa kilometa 75 ambapo utapata
fursa ya kuvuka mto Pangani kwa feri huku ukiangalia
madhari nzuri ya mji wa Pangani. Pia kuna usafiri wa ndege ambao unaweza kuandaliwa
kwenda kiwanja kidogo cha Mkwaja au Saadani.
Tofauti na hifadhi nyingine, mbuga ya Saadani inahifadhi
mali kale na wanyama wengine wa majini. Wageni mbalimbali wa ndani na nje ya
nchi hutembelea eneo hili ili kujionea maliasili zilizopo sambamba na mandhari
nzuri ya hifadhi yenyewe.
Hifadhi hii ni hifadhi
pekee ya wanyama nchini Tanzania inayopakana na Bahari (bahari ya Hindi) ina fukwe nzuri, jambo linaloifanya
iwe ya kuvutia kwa vile ni rahisi kuona
wanyama wakivinjari katika fukwe za bahari.
Mbali na
upatikanaji wa wanyama kama Parahala
hifadhi ina wanyama wa aina nyingi wa baharini na nchi kavu wakiwemo kasa wa
kijani, nyangumi wenye nundu na pomboo.
Hifadhi hii inapokea watalii wa ndani na kutoka nje ya nchi. Nyumba za wageni za TANAPA
na vibanda vinapatikana katika kijiji cha Saadani na Makao makuu ya Hifadhi , Mkwaja
Wilayani Pangani japo pia kuna maeneo mengi ya kupiga mahema .
Vile vile Serikali
kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imewezesha kuwepo kwa hoteli nzuri za
kitalii ikiwemo hoteli iliyobeba jina la mbuga ya Saadani inayojulikana kwa
jina la “Saadani park hotel”zenye huduma na mazingira mazuri.
Saadani park Hotel
Mimi ni mtanzania naitaji kutembelea hifadhi hii je utaratibu upoje kwa ujumla mpaka malazi
ReplyDelete