Taarifa Kwa Umma Juu Ya Hali ya Upatikanaji Maji Safi katika Mkoa Wa Tanga





JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 

                                

 
 
 




 
Simu:  027 2642421                                                                Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Simu Fax:   027 2647752                                                                                   S. L. P. 5095          
 E-mail: rastanga@pmoralg.go.tz                                                                          TANGA     







                                
Taarifa Kwa Umma

Mkoa wa Tanga una eneo la kilomita za mraba 27,920; kati ya hizo 572 (2.1%) zimefunikwa na maji na zilizobaki ni nchi kavu (Mpango wa Uwiano, Tanga 2011/12 – 2015/17). Kiutawala Mkoa umegawanyika katika wilaya 8 ambazo ni: Tanga Jiji, Lushoto, Korogwe, Muheza, Pangani, Handeni, Mkinga na Kilindi. Aidha, Kiutendaji kuna Mamlaka za Serikali za Mitaa 11 zenye wakazi 2,045,205 (sensa, 2012). 
 

Kijiografia Mkoa wa Tanga umepakana na Bahari ya Hindi (Mashariki), Nchi ya Kenya (Kaskazini), Mikoa ya Kilimanjaro na Manyara (Magharibi) na Mikoa ya Morogoro na Pwani (Kusini) 

UPATIKANAJI WA MAJISAFI

Mkoani Tanga utoaji huduma ya majisafi hufanywa na idara za maji za Halmashauri za Wilaya,  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mijini na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Bomba Kuu la Handeni (Jedwali 1).

Jedwali 1: Utoaji M huduma ya maji Mkoani Tanga (Machi, 2014)


NA

Wilaya

VIJIJINI

MJINI

1

 

Lushoto

H/W Lushoto

Lushoto WSSA

H/W  Bumbuli

Hakuna Mji

2

Korogwe

H/W Korogwe na HTM WSSA (kwa sehemu)

Korogwe WSSA

Mombo WSSA

3

Handeni 

H/W Handeni na HTM WSSA

Handeni WSSA

4

Tanga Jiji

H/jiji laTanga

Tanga UWSA

5

Pangani

H/W Pangani

Pangani WSSA

6

Muheza

H/W Muheza

Muheza WSSA

7

Mkinga

H/W Mkinga

Mji Kasera hakuna Mamlaka

8

Kilindi

H/W Kilindi

Songe  WSSA

           

Hadi kufikia mwishoni wa Machi, 2014 wastani wa upatikanaji wa majisafi yaliyoboreshwa ni: 51.9% (vijijini), 94.5% (jijini Tanga), 47.7% Miji Mikuu ya Wilaya na 41% mji mdogo wa Mombo (Jedwali 2).  

Jedwali 2: Wastani wa upatikanaji wa maji Mkoa wa Tanga Machi, 2014


NA

HALMASHAURI

WAKAZI  (2012)

ASILIMIA (%)

WENYE MAJI

1

TANGA Jiji (vijiji)

60,133

76

              45,701

2

PANGANI DC

44,788

57

              25,529

3

MKINGA DC

115,065

54.8

               63,056

4

MUHEZA DC

173,627

62.2

             107,996

5

LUSHOTO DC

304,246

54.8

             166,727

6

KOROGWE DC

204,337

48

               98,082

7

KOROGWE TC

27,043

45

               12,169

8

HANDENI DC

276,645

56.1

             155,198

9

HANDENI TC

44,384

59.2

               26,275

10

BUMBULI DC

160,005

25

               40,001

11

KILINDI DC

272,032

48.9

             133,024

JUMLA

1,682,305

51.9

873,758

TANGA JIJI

213,199

94.5

201,473

1

PANGANI MJI

9,237

45

 4,157

2

KASERA MJI

3,000

10

   300

3

MUHEZA MJI

30,834

17

 5,242

4

LUSHOTO MJI

28,190

62

 17,478

5

KOROGWE MJI

41,265

65

  26,822

6

MOMBO MJI

19,154

41

     7,853

7

HANDENI MJI

34,672

53

    18,376

8

SONGE MJI

14,801

42

      6,216

 

Jumla

181,153

47.7

86,444


MIRADI YA MAJI

Kati ya Januari - Machi, 2014 Halmsahauri ziliendelea kutekelezaji miradi ya vijiji kumi chini ya program ya maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP). Jumla ya vijiji 106 vyenye wakazi 265,878 (sensa 2012) vilikuwa  na miradi iliyokuwa inayotekelezwa (Jedwali 3).
 

Jedwali 3: Miradi ya vijiji 10 Mkoani Tanga


NA

H/MASHAURI

VIJIJI

WAKAZI

1

Tanga CC

10

18,193

2

Lushoto DC

14

48,678

3

Korogwe  DC

10

21,369

4

Muheza DC

10

13,389

5

Bumbuli DC

9

23,457

6

Pangani DC

10

20,523

7

Handeni DC & TC

17

47,810

8

Kilindi DC

15

34,874

9

Mkinga DC

10

11,993

10

Korogwe  TC

10

25,592

 

JUMLA

106

265,878


Hadi kufikia Machi, 2014 jumla ya miradi 17 ilikuwa imekamilika. Kukamilika miradi hiyo kumewezesha vijiji 21 vyanye wakazi 44,557 kupata majisafi na salama karibu na makazi yao (jedwali 4).
 

Jedwali 4: Miradi ya vijiji 10 Mkoani Tanga iliyokamilika Machi, 2014


 Na

H/W

Mradi

Vijiji

Wakazi

1

Lushoto DC

Irente

Irente Juu

            535

Irente  Shamba

            309

2

Korogwe TC

Kwamndolwa

Kwamndolwa

         2,799

Kwameta

Kwameta

         1,125

3

Muheza DC

Ubembe

Ubembe

         1,662

Nkumba Kisiwani

Nkumba Kisiwani

         1,091

Kibanda Nkumba

Kibanda Nkumba

            832

Kwemhozi

Kwemhozi

         1,747

4

Bumbuli DC

Bumbuli

Bumbuli Mission

         1,694

Bumbuli Kaya

         1,785

Kwemanolo

         1,529

Kweminyasa

Kweminyasa

         2,577

5

Pangani DC

Madanga na Bweni

Madanga

         1,645

 

Jaira

            577

 

Bweni

         1,263

6

Handeni DC/TC

Misima

Misima

         3,578

Suwa Kwekoma

Suwa Kwekoma

         6,592

Suwa Wimba

Suwa Wimba

         1,000

7

Kilindi

Kikunde

Kikunde

         6,093

Negero

Negero

         3,335

8

Mkinga

Daluni-Kibaoni

Daluni-Kibaoni

         2,789

 

Jumla

17

21

      44,557

 
TEKELEZA SASA KWA MATOKEO MAKUBWA (BRN)

Chini ya mfumo wa tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (Big Results Now - BRN), miradi inayotekelezwa chini ya WSDP itakamilika kabla au ifikapo Desemba, 2014. Kukamilika Kwa miradi hiyo kutaongeza idadi ya wakazi watakaopata maji vijijini kufikia 1,139,636 ambayo ni sawa na 67.7% ya wakazi wote waishio vijijini.
 

Imetolewa na

Eng. Ephraim Bariki Minde,

Katibu Tawala Msaidizi- Idara ya Huduma ya Maji,

Secretarieti ya Mkoa ,

Tanga.

 
               



Written by

1 comment:

  1. samahani kama nataka kutuma maombi ya kusoma kwa vitendo katika maabara ya maji katika wilaya ya korogwe nitapata sehemugani?

    ReplyDelete