Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Kitaifa yafanyika Wilayani Korogwe Mkoani Tanga
Siku ya wazee duniani imefanyika
kitaifa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga na
kuhudhuriwa na mamia ya wazee na wananchi kwa ujumla. Mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo ni Mhe. Dk Mohamed G. Bilali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Pamoja na mgeni rasmi pia viongozi mbalimbali wa
kiserikali wa ngazi ya kitaifa na kimkoa wamefika katika maadhimisho hayo
akiwemo Mhe. Aggrey Mwanri, Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI, Mhe. Seif S.Rashid,
Naibu Waziri wa Afya, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wakuu wa Wilaya za Tanga, Wabunge,
Viongozi wa CCM, Viongozi wa dini na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa.
Siku ya wazee
duniani huadhimishwa kila tarehe mosi mwezi wa Octoba ikiwa ni siku iliyotengwa
rasmi kwa ajili ya kutafakari mahitaji
na umuhimu wa wazee katika jamii. Kauli mbiu ya siku ya wazee mwaka huu
nchini ni “Matarajio ya wazee ni
heshima, usalama na maisha mema” Nayo Serikali imewahakikishia wazee maisha mema na imeahidi kuzimamia zoezi la upatikanaji wa huduma za afya bure bila usumbufu.
Mhe. Chiku Gallawa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Bilali mara tu baada ya kuwasili uwanja
wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kubariki maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo yanafanyika Korogwe
Serikali
inatambua umuhimu wa wazee katika jamii bila ya kujali rangi, kabila wala
itikadi za dini. Mhe. Bilal akisalimiana na Mzee ambaye ni kada wa Chadema
Maadhimisho
ya siku ya wazee duniani kitaifa Korogwe yamepambwa na mvua kubwa lakini wazee hawakuwa
nyuma kusherekea siku yao hii muhimu. Pichani ni maandamano ya wazee kuelekea
uwanja wa sherehe
Mzee
Clement Nsherenguzi mwenye umri wa miaka
77 ambaye ni mwandishi wa radio Fadeko
na radio Karagwe akiwa kazini kuchukua
matukio. Mzee huyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Saidia Wazee anaungana
na wazee wengine nchini kuiomba serikali kuendelea kupigani maslahi ya wazee
Ulifika muda wa wazee kuburudika na vikundi mbalimbali vilipamba maadhimisho hayo
Ulifika muda wa wazee kuburudika na vikundi mbalimbali vilipamba maadhimisho hayo
Baadhi
ya wazee na wananchi wa kawaida waliofika Korogwe katika maadhimisho ya siku ya
wazee duniani
Wazee
wamepata fursa ya kupima afya zao kwa magonjwa yasiyoambukizi. Pichani ni mzee
akipima uzito na presha
0 comments: