KATIBU TAWALA MSAIDIZI MKOA WA TANGA AWAASA WAHITIMU MAHAFARI YA 19 YA CHUO CHA UALIMU ECKERNFORDE.
Bi. Monica Kinara, Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundo Mbinu akiwa mgeni rasmi katika mahafari hayo akitoa hotuba kwa wahitimu wa ngazi
ya cheti na stashahada katika sherehe za maafari ya 19 ya chuo cha Eckenford
yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho aliwataka wahitimu
kujiendeleza zaidi kielimu ili
kukabiliana na changamoto za ajira nchini.
Ngoma ya asili kutoka
katika kikundi cha “Mapambano Ngoma Group” ikitumbuiza kwenye mahafari hayo.
Mkuu wa chuo cha
ualimu Eckenford Bw. Dominick Kato alimkabithi Bi Monica Kinara ripoti juu ya
mafanikio na changamoto katika taasisi hiyo.
Wahitimu wa ngazi ya cheti na stashahada katika mahafali hayo.
0 comments: