Uwekezaji Kwenye Kilimo cha Maembe Kunufaisha Wakazi wa Wilaya ya Kilindi
Wakazi wa Kilindi
wanatarajia kunufaika na kilimo cha maembe mafupi yanayozalisha maembe mengi,
makubwa na kwa wakati mfupi na lengo likiwa ni kulipatia zao hilo dhamani.
Awali Wilaya ya Kilindi imekuwa yenye mafanikio makubwa katika uzalishaji wa
maembe ya asili lakini kuna changamoto ya matumizi ya sayansi katika kilimo.
Akizungumza na timu ya uandaaji wa Makala ya
maeneo ya Uwekezaji katika Mkoa wa Tanga, Mhe. Seleman Salum Liwowa ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi amesema kuwa, baada ya kuona fursa ya ardhi yao yenye
kustawisha maembe kwa wingi, waliamua kubuni mradi wa maembe mafupi ili
kunufaisha wananchi wengi zaidi.
“Kwa sasa tumetenga eneo
la Sangeni lenye hekali 960 na tumeanza kumpatia kila mkulima aliye kwenye
kikundi cha ushirika hekali 1 , miche kwa ajili ya zoezi hilo na tayari tumeshaotesha
miche kwa ajili ya shamba la mfano ” alisisitiza afisa mipango wa Halmashauri
ya Kilindi Bw. Simon Vedastus Mzee.
Vilevile imeelezwa kuwa
lipo soko la kutosha kwani maembe ya Kilindi yanapendwa sana na soko kubwa
linapatikana upande wa Mashariki ya Kati. Miundo mbinu mizuri imesaidia
wanunuzi kufika katika Wilaya ya Kilindi kwani kuna barabara nzuri zinazofikika
kwa urahisi ,nishati ya umeme na mawasiliano.
Mhe. Liwowa anatoa wito
kwa wawekezaji wa ndani na nje kufika katika Wilaya yake na kushirikiana na Wakazi
wa Kilindi kulipatia zao hili dhamani kwa kujenga viwanda ambayo vitaweza
kusindika maembe na kutengeneza juice na kuleta utaalamu na vifaa vya kisasa
ili kurahishisha ukulima wa zao la embe.
Wilaya ya Kilindi ipo
ndani ya mwinuko na ina hali nzuri yenye ubaridi, mvua za wastani, udongo wenye
rutuba na upatikanaji wa maji na madini mbalimbali. Pia uwekezaji unaweza
kufanyika katika uzalishaji wa viungo, utalii katika maeneo ya milima ya Nguu,
Mlima wa Kilindi na poli la Handeni.
Kwa taarifa zaidi juu ya
fursa za uwekeza katika wilaya ya Kilindi tembelea tovuti ya Mkoa wa Tanga www.tanga.go.tz kisha chagua wilaya ya Kilindi na pia unakaribishwa kwenye Jukwaa la Uwekezaji kanda ya Kaskazini litakalofanyika katika Mkoa wa Tanga septemba 26-21 mwaka huu. Kushiriki Jukwaa la Uwekezaji tembelea tovuti ya uwekezaji www.investnorthernzone.go.tz na jaza form maalumu.
Mhe. Seleman Salum Liwowa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Kilindi
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kilindi
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi
0 comments: