Mkoa wa Tanga umekuwa
mwenyeji wa maadhimisho ya Kitaifa ya Utepe Mweupe wa Uzazi salama yaliyofanyika Machi 15 mwaka huu. Wiki ya
Utepe mweupe ilianza tarehe 10 ambapo iliambatana na shughuli mbalimbali
zilizolenga kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinavyozuilika vinatokomezwa.
Katika Kupata sauti za
Wananchi, Wakazi wa Wilaya tano za Mkoa wa Tanga ambazo ni Kilindi, Handeni,
Korogwe, Muheza na Jiji la Tanga walipata fursa ya kutoa maoni yao wakiwawakilisha
Watanzania jinsi gani huduma za afya
ziboreshwe kwa lengo la kupunguza vifo
vya mama na mtoto.
Uhamasishaji
wa wananchi ulifanyika kupitia vyombo mbalimbali ya habari. Pichani Bi. Agness Mbwana
ambaye ni Mratibu wa Utepe Mweupe Mkoa wa Tanga akizungumza na wananchi juu ya ushiriki wao katika
maadhimisho hayo kupitia radio ya Breeze Fm iliyoko Tanga
Dr
Herriet Mwakilishi kutokaChama cha madaktari Wanawake Tanzania ( MEWATA ) akifafanua kuhusu dalili za awali za ugonjwa
wa saratani ya matiti na huduma za
upimaji wakati wa wiki ya maadhimisho ya
Utepe Mweupe Mkoani kupitia radio ya Breeze Fm
Vikao
vya maandalizi ya Utepe Mweupe viliendelea katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Tanga ili kufanikisha zoezi la
maadhimisho kitaifa. Wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dr Asha
Mahita akifafanua jambo wakati wa kikao
Baadhi ya wajumbe wa vikao vya maandalizi
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula Said Magalula akizungumza na Waandishi wa Habari
ofisini kwake siku mbili kabla ya Kilele
cha Maadhimsho ili kuutaarifu umma kuwa
Mkoa ulijiandaa vyema na maandalizi yalikamilika tayari kwa maadhimisho ya siku
ya Utepe Mweupe kitaifa Mkoani Tanga
Baadhi ya waandishi wakati wa mkutano
Zoezi
la Upimaji wa dalili za awali ya saratani ya matiti liliiendelea . Pichani
akinamama wakisubiri kumwona mtalaamu
Read more