Bodi Ya Barabara Mkoa wa Tanga Yaonya Uharibifu Wa Barabara
Wajumbe wa Bodi ya
Barabara Mkoa wa Tanga wamesikitiswa na
baadhi ya tabia za Wakazi wa Tanga ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakifanya
uharibifu katika barabara hasa zile zenye lami. Hayo yamebainika katika kikao
cha pili cha bodi ya barabara kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mku wa Tanga siku ya alhamisi ya
Machi 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
Akifungua kikao hicho Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, magalula Said Magalula amesema lengo la kikao cha bodi ya
barabaraa ni wadau kupata habari sahihi ya uboreshaji wa barabara katika
kupunguza umaskini na kuleta maendeleo kwa wananchi.
“ Tukiweka maazimio mazuri
yanayotekelezeka barabara zetu zinaweza
kuwa katika mazingira mazuri na kuhudumia ipasavyo “alisisitiza Magalula
Pia Mhe. Magalula
alielekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za tanga kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya kutumia vivuko
vilivyowekwa barabarani rasmi kwa ajili ya kuvusha mifugo.
Kikao kiliazimia kuhakikisha uboreshaji katika kudhibiti uzito
na mifugo kutembea barabarani.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga , Mhe Magalula Said Magalula akifungua rasmi kikao cha Bodi ya
barabara
Meneja
wa TANROADS Mhandisi Alfred Ndumbaro Akitoa taarifa ya hali ya barabara katika
Mkoa wa Tanga
Mbunge
wa jimbo la Tanga Mhe Omari Nundu
akichangia mada wakati wa Kikao
Baadhi
ya wajumbe wa bodi ya Barabara na waalikwa
0 comments: