MAKAMU WA RAIS MHE. DKT MOHAMED GHALIB BILLAL AZINDUA MRADI WA KANDA MAALAMU YA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA VIWANDA PONGWE - TANGA

Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania azindua Mradi wa Kanda Maalum ya Uwekezaji katika eneo la Viwanda Pongwe. Eneo la viwanda Pongwe lipo nje kidogo ya Wilaya Tanga, mkoani Tanga.
Eneo hilo lina Ukubwa wa eneo la mradi hekta 67.7 kwa eneo la Viwanda na hekta 4.3 kwa eneo la makazi.
Mradi huu wa Kanda Maalum ya Uwekezaji ni Mradi ulioanzishwa na Tanga Economic Corridor Ltd (Industrial Park Developer) ambayo ni Kampuni inayoundwa kwa ubia kati ya  Halmashauri ya Jiji la Tanga yenye hisa 49% na (Good PM Group Ltd through Africa Future) yenye hisa 51%) ambayo ni Taasisi isiyo ya Kiserikali kutoka nchini Korea inayowezesha uendelezaji wa miundo mbinu Afrika.  Makubaliano yaliyopo ni Halmashauri ya Jiji la Tanga kuchangia eneo na Good PM Group Ltd kuwekeza katika miundombinu.  Mradi mzima unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 277 ambapo milioni 40 zitatumika kwa kuendeleza miundombinu na dola za Kimarekani milioni 237 zitatumika kwa Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa viwanda vyote.
 Baada ya mradi huu kukamilika unatarajiwa kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi ya 2,000 katika viwanda 17 vinayotarajiwa kujengwa.


  Mhe. Makamu wa Rais akivishwa skafu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mkoani Tanga.
 Mhe. Mkuu wa Mkoa Tanga (Mwenye kilemba kichwani) akimuongoza Mhe. Makamu wa Rais akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika kumpokea.
 Mhe. Makamu wa Rais akisaini kitabu cha wageni kulia ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Chiku Galawa (Mwenye kilemba kichwani) na  kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Abdalah Kigoda 
(mwenye miwani aliyekaa).
 Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Chiku Galawa akitoa salamu na kutambulisha wageni waliohudhuria.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisalimia.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendegu akisalimia.
 Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor Bw. Chriss akisoma hotuba .
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Abdala Kigoda akisoma hotuba fupi kabla ya kumkaribisha 
Mgeni Rasmi Mhe. Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais Mhe. Mohaned Billal akisoma hotuba ya ufunguzi.
 Mhe. Makamu wa Rais akizinduwa rasmi jiwe la msingi.
 Mhe. Makamu wa Rais akipanda mti.
 Mh. Makamu wa Rais akizinduwa rasmi ujenzi wa viwanda.
Mhe. Makamu wa Rais (wa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliofika katika uzinduzi huo.


Written by

0 comments: