Wafugaji Watakiwa Kufuata Taratibu Za Kupata Ardhi


Wafugaji wa Jamii ya Kimasai wanaoingia kwenye wilaya ya Handeni mkoani Tanga wametakiwa kufuata taratibu mzuri za kupata ardhi kihalali kuliko kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyopo kisheria jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa mvutano wakati wanapotakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ambapo alisema kutokufuata taratibu za upatikanaji wa maeneo wanaoyoishi kumekuwa kukisababisha migogoro isiyokuwa na tija jambo ambalo linarudisha nyuma`maendeleo.

Alisema kuwa kimsingi lazima wanapotaka ardhi kwenye maeneo wanayokwenda wafuate utaratibu kwa kuanzia ngazi za chini kupitia serikali za vijiji kwenye mikutano yao ambayo itawafanya wao kufanikisha matakwa yao badala ya kukubali kupewa kienyeji.

Hatua hiyo ya Mkuu huyo wa mkoa inatokana na wananchi wa jamii ya kimasai wanaoishi kwenye kijiji cha Kwamatuku Kata ya Kwamatuku wilayani hapa kumuonyesha mabango  mbalimbali waliyokuwa wameshikilia wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara kwenye shule
yasekondariyaKwamatuku.

Akiwa shuleni hapo akiendelea na ukaguzi huo ndipo wananchi hao walipofika ambapo mmoja wao Nalepo Lengai alimueleza RC Gallawa kuwa shida yao kubwa iliyowapeleka eneo hilo ni kuwa wanateseka baada ya kuchomewa nyumba zao walizokuwawakiishikwenyeeneohilo.

Baada ya kauli hiyo mkuu huyo wa mkoa aliwataka wamueleze walifanyiwa vitendo hivyo na wakina nani ambapo walishindwa kujibu kutokana na kuwa eneo ambalo walikuwa wakiishi lilikuwa la hifadhi na sio makazi ya watu.
 “Nani amewachomea nyumba kwani nyie hamfahamu kuwa kuishi ndani ya hifadhi ni kosa sasa kwanini mnashindwa kufuata taratibu za matumizi bora ya ardhi hivyo nawasihi hakikisheni mnafuata utaratibu uliopo “Alisema RC Gallawa.

Hata hivyo alisema kuwa taratibu za upatikanaji wa ardhi hapa nchini zipo wazi na mtu hawezi kujipimia sehemu mwenyewe na kudai kuwa ni yake hasa kibaya zaidi kuuziwa ardhi eneo la hifadhi kwani ni makosa makubwa sana.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni,Muhingo Rweymamu aliwataka wananchi hao kama wameuziwa eneo hilo la hifadhi basi waende mahakamani wakamshtaki mtu huyo aliyewapa mahali hapo.

“Ninasema kama kuna mtu amewauzia ni muhuni nyie nendeni mahakamani mkamshtaki huyo mtu ambaye amewapa ardhi kwenye eneo la hifadhi mimi nitawasaidia “Alisema DC Muhingo ( Stori & picha na Osca Assenga-Handeni)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akishiriki ujenzi wa maabara kwenye shule ya sekondari Kwamatuku wakati alipoitembelea kukagua maendeleo yake

 
 
 


Written by

0 comments: