Utepe Mweupe Wakutana Na Waandishi Wa Habari Mkoani Tanga
Bi Rose Mlay, Mratibu wa Muungano wa Utepe Mweupe akitoa mada . Kulia ni Bw. Kenneth Simbaya , Mmoja wa wakufunzi kwenye warsha.
“Mama akiwa salama Taifa
liko salama, Mama anapokufa na Taifa linakufa” Hayo ni baadhi ya maneno ambayo
waliaswa waandishi wa habari kwenye warsha ya Waandishi wa habari iliyoandaliwa
na Muungano wa Utepe Mweupe iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Walemavu ( YDCP)
Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya Habari Mkoani Tanga walipata wasaa
wa kuongeza uelewa wa masuala ya Vifo vya Mama na Mtoto. Akizungumza kwa
hisia kali, Bi Rose Mlay ambaye ni
Mratibu wa Muungano wa Utepe Mweupe aliwaomba waandishi wa habari kuungana na
makundi mengine katika jamii kupaza sauti kwa niaba ya akina mama ili kupunguza vifo vya
mama na mtoto.
“Sababu za vifo vya mama
na mtoto hazichagui zinaweza kutokea kwa mama yeyote awe tajiri ama maskini.
Mama anahitaji kituo cha afya kilichokaribu na chenye huduma nzuri , vifaa na
wataalamu. Jamani Tuwajibike ili mama aishi”
Naye Bw. Kenneth Simbaya ,
mmoja wa wakufunzi kwenye warsha hiyo alitoa wito kwa waandishi wa habari kuona umuhimu wa kuandika makala na
habari za vifo vya akina mama na watoto ili jamii husika na serikali
ilichukulie suala hilo kwa uzito mkubwa.
Warsha
ya waandishi wa habari iliyoamdaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe ni maandalizi
ya maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe yenye kauli mbiu “Wajibika Mama Aishi”yatakayofanyika kitaifa Machi 15
katika Mkoa wa Tanga.
Bw. Hassan Hashim, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Tanga ambaye pia ni Mwakilishi wa
Channel Ten akichangia mada wakati wa Warsha
Bw.
John Semkande, mwakilishi kutoka Pangani
Fm akitoa ushuhuda ni kwa jinsi gani amekuwa akitimiza wajibu wake ili
kuhakikisha anaokoa maisha ya mama na mtoto
0 comments: