OCD LUSHOTO AWAASA WAENDESHA BODABODA
Mkuu wa Polisi wilaya ya Lushoto, Magafu Abdallah amesema Jeshi la Polisi wilayani humo litahakikisha linawakamata waendesha bodaboda waliopo Wilayani humo ambao watabainika wamevunja sheria za usalama barabarani kwa kupakia abiria zaidi ya mmoja na kutokuvaa kofia ngumu wanapokuwa wakiendesha.
Akiongea ofisini kwake, amesema sheria za usalama barabarani
zimeendelea kuvunjwa licha ya elimu ya
kutosha juu ya upakiaji wa abiria na kuwa na leseni za kuendesha vyombo . Kushindwa
kutimiza masharti ya usalama barabarani kumehatarisha usalama wa abiria.
“Pikipiki nyingi
hazijasalijiwa na mamlaka ya mapato nchini TRA, tumekuwa tukiwaelimisha watu
kuvaa kofia ngumu kwa ajili ya usalama wao lakini wanakuwa wabishi nadhani njia
nzuri ni kuwakamata wale wote wanaokiuka utaratibu huo ili waweze kuchukuliwa
hatua zinazostahili “Alisema Abdallah.
Hata hivyo
amesema asilimia 90 za ajali zinatokana na uzembe wa madereva wanaoendesha
vyombo hivyo kwa kutokufuata misingi na sheria ambazo zimewekwa na hivyo
kupelekea ajali za mara kwa mara ambapo aliwataka kuzingatia sheria ili
kuepukana na ajali.
Wananchi
pia wameaswa kuwa mstari wa mbele kuwasaidia waendesha bodaboda hao kufuata
sheria za usalama barabarani kwa kukataa kupanda kwenye vyombo hivyo vya
usafiri kama hawana kofia .
0 comments: