YANGA NA MGAMBO SHOOTING KUCHUANI VIKALI JUMATANO HII VIWANJA VYA MKWAKWANI
YANGA AFRICAN
MGAMBO SHOOTING
Kocha Mkuu wa timu ya
Mgambo Shooting, Mohamed Kampira amesema mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara kati
yao na Dar es Salaam Yanga African unaotarajiwa kuchezwa Jumatano tarehe 17/04/2013 saa 10 jioni kwenye uwanja
wa Mkwakwani Mkoani Tanga hauwapi wasiwasi wala kuwanyima usingizi kwani kwao wanauona kama
mchezo wa kawaida katika ligi hiyo.
Kampira aliyasema
hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yao ya asubuhi ambapo alisema
maandalizi ya mechi hiyo licha ya wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini
kuitabiria kuwa itakuwa ni ngumu lakini wao wanaiona kama yakawaida sana
kutokana na uimara wa kikosi chao.
Alisema kuwa kikosi
hicho hivi sasa kipo imara kwa ajili ya kupambana na timu yoyote ili iweze
kutimiza malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha wanamalizia ligi hiyo
wakiwa kwenye nafasi tano za juu kwenye msimamo.
Nao Umoja wa Wanachama wa Klabu ya Yanga mkoa
wa Tanga umeanza shamra shamra za kuwapokea viongozi wa timu hiyo ambao
watawasili mkoani hapa siku moja kabla ya kuchezwa mechi hiyo ambayo
inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa.
Katibu
wa Matawi ya Yanga mkoa wa Tanga,David Manyilizu alisema mapokezi ya viongozi
hao yanatarajiwa kufanyika katika njia ya Panda ya Segera wilayani Handeni na
Pongwe jijini Tanga ambapo wapenzi na wanachama wa klabu hiyo wataungana ili
kuwalaki viongozi hao
0 comments: