“RETREAT” YA UONGOZI WA KIMKAKATI KWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO YALENGA MABADILIKO YA UTENDAJI KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA TANGA NA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO.
Bw: Benedict Ole Kuyan, Katibu Tawala Mkoa
wa Tanga akitoa maada maalumu juu ya uongozi wa kimkakati wakati wa “RETREAT” ya watumishi ambao ni wakuu wa wa Idara na Vitengo iliyofanyika
kwa muda wa siku mbili wilayani Pangani . Lengo kuu lilikuwa ni kuwaleta wakuu
hao pamoja ili kupata elimu zaidi juu ya kufanya madiliko ya kuboresha utendaji
katika idara na vitengo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga na Hospitali ya Rufaa
ya Bombo.
Washiriki waligawanyika kwenye makundi
mawili na kujadili jinsi ya kuimarisha utendaji mzuri katika maeneo ya mawasiliano
na ukaguzi.
Washiriki wa “RETREAT” walipata fursa ya chemsha bongo. Kila mmoja alihitajika
kujitathimini utendaji wake kwa kujaza form maalumu ambayo ililenga kusaidia
kujua uweledi na udhaifu wa kila mmoja ili kutafuta namna ya kujirekebisha.
Washiriki wa “RETREAT” wakisikiliza mojawapo ya maada zilizotolewa kwa makini.
Picha ya pamoja ya KatibuTawala Mkoa wa Tanga ( wa nne kulia) pamoja na Wakuu wa Idara na
Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga na Hospitali ya Rufaa ya Bombo.
0 comments: