TANGA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU 2013 KESHO TAREHE 16/05/2013

Wakazi wa Tanga wako kwenye shamrashamra na maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru  unaotarajiwa kuingia hapo kesho saa 2.00 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi anatarajiwa kumkabithi Mkuu wa Mkoa wa Tanga
 Mhe. Chiku Gallawa Mwenge huo  tayari kukimbizwa katika wilaya zote  nane (8).
Mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, zimebeba ujumbe usemao: “Watanzania ni  Wamoja” wenye kauli mbiu “ Tusigawanywe kwa misingi ya Tofauti zetu za Dini, Itikadi, Rangi na Rasilimali” Lengo la Ujumbe na Kauli Mbiu hii ni kutoa msisitizo kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kuimarisha Umoja  na Amani katika jamii .Miradi mbalimbali ya maendeleo itawekewa Mawe ya Msingi, kufunguliwa na Kuzinduliwa ikiwa jumla ya miradi 51 yenye  thamani Shilingi Ishirini na saba bilioni mia tisa themanini milioni mia sita na moja elfu mia nne arobaini na nne (27,980,601,444)
Baada ya kupokelewa ki Mkoa utakabithiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego na siku inayofuata utaelekea  Wilaya ya Mkinga, Muheza, Pangani, Handeni, Kilindi, Korogwe,Lushoto na tarehe 24/05/2013 utakabithiwa  kwa Mkoa wa Kilimanjaro katika kijiji cha Bendera  Same.


Written by

0 comments: