Ma-Dc Tanga waagizwa kuhamasisha Wakulima kuweka akiba ya Mavuno
Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Chiku Gallawa amewaagiza WAKURUGENZI
watendaji pamoja na wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoa wa Tanga kupeleka maelekezo katika vijiji vyote ya kuwahimiza wakulima kuweka hifadhi ya chakula kwa kila Kaya mara baada ya kupata
mavuno mashambani msimu huu.Katika
taarifa zilizotolewa na wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya tisa zilizopo Mkoani Tanga,zimeonyesha hali ya mvua katika msimu wa masika 2013 kutakuwa na mazao mengi ya Mahindi, Mpunga, Mihogo, Maharage, Kunde, Mbaazi na mbogamboga. Hii ni dalili nzuri kwa Mkoa kwa ujumla.
Mhe. Chiku Gallawa ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga akisisitiza jambo wakati wa kuwasilishwa taarifa ya Maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na ushirika ya Mkoa.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Olekuyan
akiwasilisha vipaumbele vya Mpango wa Uwiano wa Maendeleo vya Mkoa katika
kikao cha Maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Mkoani Tanga.
Baadhi ya wajumbe Kutoka Wilaya za mkoa wa Tanga kwenye Kikao cha Maendeleo ya Kilimo
0 comments: