HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA YATOA HUDUMA YA UPASUAJI BURE
Hospitali
ya Bombo kwa kushirikiana na Madaktari wa Shirika la Interplast la Ujerumani
imeanza kutoa huduma ya bure ya upasuaji
wa kurekebisha maumbile kama kupasuka midomo ( cleft lips)
kupasuka kaakaa (cleft palate) Uvimbe ( turmors) na Makovu sugu ambayo
itakuwepo kwa muda wa siku 10.
Huduma
ya upasuaji imeanza kwa uchunguzi wa wagonjwa wenye matatizo hayo kisha
kupangiwa tarehe ambapo upasaji wa kwanza umeanza leo tarehe 16/07/2013.
Kwa
mujibu wa mratibu wa zoezi hilo la upasuaji Dr Wallace Karata, ushirikiano wa
upande hizi mbili katika kunusuru maisha ya Watanzania ulianza mwaka 2011 ambapo hospitali iliona umuhimu wa
kuwasaidia wananchi hasa wale wasio na uwezo wa kulipia upasuaji na matibabu.
Jumla ya operation 80 zilifanyika mwaka jana na mwaka huu zaidi ya wagonjwa 50
wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwa matatizo mabalimbali.
Aidha
, uandikishwaji wa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ulianza tarehe
17/6-
10/7/2013 kwa gharama ya shillingi za kitanzania elfu tano ( 5000). Jumla
ya watu wazima 65 na watoto 17 wamejitokeza
kufanyiwa uchunguzi wa awali kwa ajili ya upasuaji.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wananchi ambao wametokea pande mbalimbali za nchi ikiwemo Dar es salaam, wameishukuru Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, uongozi wake
na shirika la Interplast la Ujerumani kwa huduma hiyo muhimu.
Mtoto
Sylvesta Bulaji mwenye umri wa miaka 12 kutoka maeneo ya Mabawa Mkoani Tanga
akifanyiwa Uchunguzi katika Hospitali ya
Bombo ili kufanyiwa upasuaji wa mdomo uliopasuka kwa ndani. Miaka 10 iliyopita
alifanyiwa upasuaji wa mdomo wa nje uliokuwa umepasuka.
Mtoto
Aaliya Maeda mwenye umri wa miaka 2 ½ kutoka Dar es salaam akifanyiwa uchunguzi
wa awali wa mkono wake ulioungua vibaya na kusababisha vidole kujikunja kwa
ajili ya Upasuaji.
Baadhi
ya wagonjwa na ndugu zao waliofika katika Hospitali ya Bombo kwa ajili ya uchunguzi wa awali
0 comments: