Wilaya ya Korogwe yapongezwa kwa kuonyesha ushirikiano katika shughuli za maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Chiku Gallawa ameipongeza Wilaya ya Korogwe
kwa kuonyesha ushirikiano katika shughuli za maendeleo. Hayo ameyasema wakati
akiongea na watumishi wa Halmashauri Mji na Halmashauri ya Korogwe Vijijini
mara baada ya kuwasili Wilayani hapo jana kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na pia katika Mkutano wa
Hadhara uliofanyika katika Kata ya Mpale.
“ Nawapongeza kwa kuonesha
dalili nzuri ya ushirikiano, siri ya
yote haya ni kujituma na upendo, Hamasa yenu isiishie katika ujenzi wa maabara
bali pia tuangalie uboreshaji wa suala zima la elimu kuanzia shule za msingi
hadi sekondari” amesisitiza mkuu huyo.
Wilaya ya Korogwe imejiwekea mkakati kazi
kutekeleza agizo la kitaifa lililotolewa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete la kila
shule ya sekodari kujengewa maabara ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa masomo ya
masomo ya sayansi.
Imekubalika kuwa Mkuu wa Wilaya
atachangia bati 20, Wakurugenzi bati 10 kila mmoja ,Watumishi wa wilaya ya Korogwe kuchangia mabati moja kila mmoja , kila
kijiji kimejiwekea lengo la kuchangia matofali na mkazi yeyote mwenye kipato
kuchangia shilling elfu kumi (10,000) ili kufanikisha ujenzi huo.
Naye Mkuu wa Wilaya Mhe.
Mrisho Gamba amekiri kuwa ni wajibu wake kutekeleza maagizo ya Rais na haoni
sababu ya kutafuta visingizio vya kutojenga maabara kama ilivyoagizwa na Mhe.
Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuboresha sekta ya Elimu nchini.
“Sisi Wilaya ya Korogwe
tumezingatia maagizo ya Rais na Maelekezo yako Mkuu wa Mkoa na kuamua
kuhamasishana ili kujenga maabara na kazi hiyo tumeianza kwa kazi ya ajabu”
aliongezea Mhe. Gambo.
Hata hivyo tayari ujenzi
umeshaanza Kata ya Mpale na Mkuu wa Mkoa amefanikiwa kuzindua ujenzi wa maabara
ya vyumba vitatu katika shule ya sekondari Patema iliyopo kata ya Mpale mbavyo
msingi wake ulishachimbwa.
Wakiunga mkono juhudi hizo,
Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Gallawa ameahidi kuchangia shilingi milioni mbili, Mbunge
wa Korogwe vjijini Mhe. Steven Ngonyani Majimarefu amechangia fedha taslimu laki tano na Kampuni ya Katani
imechangia bati 20 na na misumali.
Akiupongeza uongozi wa
Wilaya ya Korogwe kwa mikakati mizuri wakati wa Mkutano wa hadhara, mkazi wa
kijiji cha Patema Kata ya Mpale
Bw.Omari Baruti amesema maendeleo ya nchi huletwa na mwananchi mwenyewe kwa kujituma
hivyo yuko tayari kushirikiana na kijiji katika kutimiza azama yake ya ujenzi
wa maabara.
Nao wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Patema kata ya Mpale ambapo ndiko ujenzi wa maabara umezinduliwa,
wamefurahishwa na juhuzi hizo za serikali kwani wanaona kuwa maabara hizo
zitakuwa mkombozi kwa wanafunzi wa sayansi ambao wana changamoto ya kusoma bila
vitendo.
Mkakati wa kushirikiana
kuleta maendeleo katika Wilaya ya Korogwe unahamasishwa na msemo usemao Panga, tekeleza ,onesha Mafanikio na Hakuna
kulala hadi kieleweke”
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Gallawa kuongea na
watumishi wa Halmashauri za Wilaya
Mwakilishi
wa Kampuni ya Katani Bw. Grayson Mmyari akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Gallawa mabati 20 na misumari kwa ajili ya
ujenzi wa maabara
Mbunge
wa Korogwe Vijijini Mhe. Steven Ngonyani akitoa mchango wa shiling laki tano kwa ajili ya
ujenzi wa maabara
Baadhi
ya Watumishi kutoka Halmashauri za Korogwe Mji na Vijijini
0 comments: