Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini Lafana
Mwenyeji wa Kongano la uwekezaji la Kanda ya Kaskazini Mhe. Chiku Gallawa , Mkuu wa Mkoa wa Tanga ( kushoto) akimwongoza mgeni rasmi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Kongano ulioko Mkonge Hoteli . Kongano hili linafanyika katika jiji la Tanga na limelenga kukuza uchumi na kuongeza ajira katika Kanda ya Kaskazini.
Mhe. Mizengo Pinda akifungua rasmi Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini. Amesisitiza kuwa kuwekeza ni lazima iwe ni kwa wananchi wenyewe au kwa kukaribisha wageni kutoka nje ya eneo husika." Hakuna nchi yeyote yenye maendeleo ambayo haina wawekezaji aidha wa ndani au wa nje" alisema Mhe.Pinda.
Baadhi ya wageni/wawekezaji waliofika katika Kongano. Zaidi ya wageni 450 wamefika kujionea fursa za uwekezaji zilizopo katika Kanda ya Kaskazini.
Halmashauri kutoka Mikoa ya Kanda ya kaskazini zilikuwa tayari kupokea wageni /wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali. Mabanda ya kila Halmashauri yamepambwa na kila aina ya vipeperushi, makala kuelezea na kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo. Mhe. Pinda akitembelea moja kati ya mabanda ya Halmashauri.
Mgeni/Mwekezaji akipata maelezo kutoka banda la Halmasahuri ya Muheza, moja kati ya Halmashauri za Mkoa wa Tanga.
Baadhi ya Mazao na madini yanayopatikana katika Mkoa wa Tanga. Tanga ni mmojawapo ya Mikoa ya Kanda ya kaskazini yenyeardhi yenye rytuba inayofaa kwa kilimo cha matunda, mazao ya chakula na biashara na pia inayopatikana madini yenye thamani kubwa
Kila mgeni alifanikiwa kupata mifuko hii iliyotengenezwa na zao la Mkonge na ndani yake kulikuwa na notibook, kalamu na Tshirt. Mkonge ni zao maarufu linalolimwa katika Mkoa wa Tanga. Mashamba mengi ya Mkonge yaliyokuwa yametelekezwa sasa yameanza kufufuliwa upya na ni lengo la Mkoa wa Tanga kurudisha hadhi ya zao hili.
0 comments: