WAJUMBE WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA WATEMBELEA OFISI YA MKUU WA MKOA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Chiku Mgallawa akutana na wajumbe wa tume ya kurekebisha sheria ofisini kwake ambao
wamefika katika Wilaya ya Tanga kwa lengo la kuzungumzia masuala ya mapitio ya
sheria mbalimbali zikiwemo sheria ya Ardhi, maisha ya wazee, mchakato wa
kupitia sheria ya haki za walaji pamoja nasheria ya makosa ya jinai.
Ujumbe huo ambao
umeongozwa na mwenyekiti wa tume Bw. Aloyious Mujulizi umefika mkoani Tanga kwa
ajili ya kikao cha wafanyakazi kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mapitio ya
sheria ya migogoro ya ardhi. Naye Katibu
Tawala mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan
alipotembelewa ofisini kwake amesema
kuwa kikao hicho ni muhimu sana kwa sababu Tanga ni mojawapo ya mikoa
inayokabiliana na changamoto ya migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji
Akizungumzia mafanikio na
changamoto za Mkoa wa Tanga Mhe. Gallawa amesema kuwa Mkoa wa Tanga una shughuli nyingi za
maendeleo ikiwemo kilimo na ufugaji, Utalii, pamoja na Mawasiliano na Uchukuzi.
Kwa upande wa utalii kuna maeneo ya magofu, Mapango ya Amboni pia kuna hifadhi
za Wanyama pori kama Saadani ambavyo kwa pamoja huvutia watalii.
Vilevile Mhe.
Gallawaamezungunzia mawasiliano na uchukuzi na kuonesha hatua kubwa kwenye Miundo mbinu
bora ya usafirishaji akijumuisha barabara, Reli na kiwanja cha Ndege ambacho
kwa sasa idadi ya abiria wanaosafiri kwa Ndege hufikia 250 kwa siku. Hilo ni
ongezeko kubwa ukilinganisha na miaka nyuma. Lakini pia amezungumzia usafiri wa
Majini kutoka Bandari ya Tanga na Kuingia umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Pia amesisitiza nia ya
serikali katika kunufaisha wananchi na ardhi yao hasa katika uwekezaji ambapo wawekezaji na wananchi huingia ubia
badala ya kuchukua ardhi . Hii ni kwa kufuata utaratibu na kulinda mali za
wananchi.
Mhe. Gallawa aliwataka wajumbe wa tume ya
marekebisho ya sheria kusaidiana na Serikali katika changamoto ya kutatua
migogoro ya Ardhi ambayo huchelewa kufanyiwa ufumbuzi, mapitio ya Sheria ya Ardhi
lazima yaendane sawa na uhifadhi wa mazingira.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan
(katikati) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Utawala
na Rasilimali watu ( kulia) ofisini kwake. Kushoto ni Afisa Habari wa Tume
Katibu Mtendaji
wa tume Bi. Winfrida Korosso
akikabidhi nakala za vitabu vya mapitio ya mfumo wa sheria zinazohusu
utatuzi wa migogoro ya ardhi 2013 kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan.
0 comments: