Kikao cha Wadau wa Uchukuzi Kujadili Mpango wa Serikali Kwenye Sekta ya Uchukuzi Katika Mkoa wa Tanga

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dr Harison Mwakyembe na mwenyeji wake Mh. Chiku Gallawa wakisikiliza hoja katika kikao hicho. Hoja nyingi zimesisitiza uboreshaji wa miundo mbinu katika Bandari , Reli na Kiwanja cha ndege ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na wananchi.

Naye Mhe. Mwakyembe ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje kuona haja na mahitaji yaliyopo sasa katika   uwekezaji katika Reli, Bandari na Uwanja wa ndege. Amesema ambaye yuko tayari anakaribishwa ili kuunga mkono juhudi za serikali katika uboreshaji wa Miundombinu ya uchukuzi. “ fursa ziko nyingi , kwa mfano kuwekeza katika meli kusafirisha wananchi kutoka Tanga kuelekea Zanzibar na Pemba na pia kwenda Dar es salaam, hiki sio kipindi cha kutumia majahazi” Mhe. Mwakyembe amesisitiza.


Baadhi ya wadau wa uchukuzi  wakisikiliza hoja za kikao . Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid H. Mwanga na kushoto kwake ni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga
Wadau wa uchukuzi kutoka sehemu mbalimbali wakisikiliza hoja


Baadhi ya wadau wa uchukuzi wakibadilishana mawazo mara baada ya kikao. Wa Kwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan akiwa na Mkurugenzi wa MWAPORC Bw.Beenunule E. Nunumisa.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Ndedego  (kulia) akiwa na wadau wengine
Wadau kutoka sehemu mbalimbali
Mhe.Subira Mgalu , Mkuu wa Wilaya ya Muheza ( Kushoto) akibadilishana neno  na Mdau
Mhe.Mboni Mgaza , Mkuu wa Wilaya ya Mkinga (kulia) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Bi.Amina Kiwanuka (katikati)  na Bi Monica Kinara ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu.
Wadau wa Uchukuzi kutoka pande mbalimbali


Written by

0 comments: