Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa Akabidhi Zawadi za Eid –Elhaji kwa Wazee na Mahabusu ya Watoto
Mhe. Chiku Gallawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga akimkabidhi
Msimamizi wa Mahabusu ya watoto Bi. Ng’wanza John zawadi za Eid-Elhaji ambazo
zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKt Jakaya Mrisho
Kikwete katika mahabusu iliyopo barabara ya 15 na 16 Jijini Tanga leo. Mahabusu
hii ni mojawapo ya mahabusu tano za watoto zilizopo Tanzania na lengo ni
kuwalinda watoto juu ya ukatili, unyanyasaji au kuiga baadhi ya tabia kutoka
katika Mahabusu za watu wazima
Wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea na wasiokuwa
na ndugu wanaolelewa katika kituo cha serikali cha kulea wazee kilichopo
Mwanzange jijini Tanga wakifurahia zawadi za Eid- Elhaji zilizotolewa na Mhe.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku
Gallawa. Kushoto ni Mhe. Halima Dendego, Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Mhe. Chiku Gallawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga akitoa
salamu za Eid –Elhaji kwa wakazi wa Tanga wakati akiongea na waaandishi wa
Habari wakati wa kukabidhi zawadi za Eid-Elhaji katika kituo cha Kulea wazee.
Amewataka wakazi wa Tanga kusherehekea sikukuu hii kwa utulivu,usalama na
kumshukuru Mwenyezi Mungu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa na Mkuu wa
Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego wakiwa katika picha ya pamoja na wazee
wanaolelewa katika kituo cha serikali cha kulea wazee.
0 comments: