Mkoa Wa Tanga Wapokea tuzo Mikoa Inayofanya Vizuri katika Sekta Ya Elimu Nchini
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akipokea tuzo ya Elimu Kwa Mkoa wa
Tanga kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga
Bw. Salum Mohamed Chima mapema wiki hii ofisini kwake iliyokabidhiwa na
Mhe. Mizengo. P. Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
wa sherehe za Uzinduzi wa Wiki ya Elimu nchini iliofanyika Dodoma Mei 2014. Mkoa wa Tanga umekuwa wa kwanza kitaifa kwa
kuwa na shule nyingi zililizofanya vizuri
mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba 2013, kidato cha nne 2013 na Kidato cha
sita 2013.
Tuzo
yenyewe; Hongera Sana Mkoa wa Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa
akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani
C. Chomola
Furaha na vifijo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wakati
wa kutolewa habari njema ya Ushindi wa Mkoa wa Tanga.
0 comments: