Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusiana Na Ugonjwa Wa Dengue Katika Mkoa Wa Tanga


 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akitoa  taarifa  kwa Waandishi wa habari  ( Hawapo pichani ) wakati wa Mkutano na vyombo vya habari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga kuhusiana na ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Tanga .Amewataka wakazi wa Tanga na wananchi kwa ujumla  kuondoa hofu ya kuwepo kwa ugonjwa huo katika Mkoa wa Tanga  kwa sababu hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuhusishwa na ugonjwa huo. Aidha Dr Asha anawasisitiza  wakazi wa Tanga kuendelea kufanya usafi katika  mazingira yote kwani ugonjwa wa Dengue huambukizwa na Mbu anaeitwa Aedes ambaye mara nyingi hupatikana  maeneo yaliyotuama maji masafi mfano kwenye ndoo za maji, vifuu, matairi ya gari n.k. Kushoto ni Afisa Habari wa Mkoa wa Tanga  Bi. Monica Laurent
 
 
Afisa Habari Mkoa wa Tanga Bi Monica Laurent akijibu moja ya maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani). Wakazi wa Tanga waelewe kuwa  tayari Mkoa wa Tanga umepokea  vipimo vya Ugonjwa wa Dengue  na kwa sasa vinapatikana katika hospitali ya Rufaa Bombo na kuna uwezekana wa kuvisambaza katika Wilaya za Mkoa wa Tanga. Ni jukumu la kila mmoja kuwahi katika vituo vya afya mara ahisipo dalili za ugonjwa wa Dengue


Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa mkutano
 
 


Written by

0 comments: