Mkutano wa 30 wa ALAT Taifa Mkoani Tanga- Muheza Yafanya Vizuri Makusanyo ya Mapato
Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mwenyekiti wa ALAT Taifa Dr Didas Masaburi mara tu baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Tanga kwa lengo la kufungua mkutano mkuu taifa wa 30 wa ALAT unaofanyika jijini Tanga katika hoteli ya Regal Naivera , Tanga. Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imetangazwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato nchini zikiwemo na Halmashauri za Kilwa, Chikonge, Tabora, Hai, Kibaha, Nombe, Temeke, Kinondoni, Lindi, Moshi na Mtwara. Mionggoni mwa Halmashauri zilizofanya vibaya ni Morogoro, Chato, Ngorongoro, Mpwapwa, Londido na Handeni.
Viongozi wa ngazi ya Mkoa wakisalimiana na Mhe. Mizengo Pinda.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Mhe. Mizengo .K.Pinda.
Wajumbe wa mkutano wasikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Pinda .
Madiwani wa Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Mizengo. K. Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania na viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na taifa.
0 comments: