Mkuu Wa Mkoa Tanga Mhe. Gallawa Atembelea Maonesho ya Pili ya Biashara Yanayofanyika Mkoani Tanga
Mhe.
Chiku Gallawa akisalimiana na Watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanga wakati akitembelea
maonesho ya pili ya Biashara yanayoendelea hadi Juni 02, 2014 katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga alasiri jana. Kwa mara
ya kwanza maonesho ya Biashara Mkoani Tanga yalifanyika Mei mwaka 2013.Akihojiwa na Waandishi wa
Habari mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho, Mhe Chiku Gallawa
ameuhakikishia umma kuwa Ulinzi na Usalama umeimalishwa na ametoa wito kwa wakazi wa Tanga na wananchi
kwa ujumla kutembelea maonesho hayo ili
kujionea bidhaa na fursa za biashara
Mhe.
Gallawa na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima (kulia mwenye
shati jeupe) wakiangalia bidhaa ya mkoba ambao umetengenezwa kutokana na
zao la Mkonge walipotembelea banda la kampuni ya Katani
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mhe. Mhingo Rweyemamu (kushoto) akifafanua jambo kuhusiana
na kilimo bora na cha kisasa cha matunda wakati Mhe. Gallawa alipotembelea
banda la wakulima kutoka Halmashauri ya Handeni
Mhe.
Chiku Gallawa akisalimiana na Meneja wa kituo cha Radio cha Breeze FM, Bi.
Agnes Mambo wakati alipotembelea banda la kituo hicho
0 comments: