Maonesho ya Pili ya Biashara Mkoani Tanga Watanzania Wakumbushwa Kupenda Bidhaa Zinazozalishwa Tanzania
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya pili ya Biashara yanayoendelea katika katika viwanja
vya Tangamano jijini Tanga. Maonesho hayo yameanza tarehe 26 Mei na
yatamalizika tarehe 02 June, 2014. Kushoto kwake ni Mhe. Halima Dendego, Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
“Si vizuri kushabikia bidhaa za kutoka
nje wakati bidhaa za aina hizo zinapatikana hapa nchini ni lazima tukuze ile
dhana ya nunua bidhaa za Tanzania Jenga Tanzania na jukumu la kujenga
nchi yetu ni la sisi sote” amesisitiza Mhe. Kigoda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Kigoda
amesema kuwa eneo la biashara na Uwekezaji ni eneo lenye fursa nyingi hivyo ni
changamoto ya kila mwananchi kujipanga kutumia ujuzi, uzoefu na ushirikiano ili
kutumia rasilimali zilizopo na kuzalisha kwa lengo la kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa
ujumla. Pia amewaasa Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa Tanzania.
Viongozi Wakuu wa Kitaifa na wa Mkoa wa
Tanga wakati wa ufunguzi
Afisa Magereza akito maelezo juu ya bidhaa
zinazotengenezwa na Magereza kwa Mhe. Kigoda
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Kigoda akiangalia jinsi zao la Mkonge
linavyoandaliwa kwa ajili ya matumizi ya bidhaa mbalimbali.
Wanahabari wakiwa kazini
0 comments: