Matangazo ya Kituo cha Televisheni cha Halmashauri , Tanga Televisheni Yarejeshwa Rasmi
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Omari Guledi Mohamed akiongea wakati wa mkutano na
Waandishi wa Habari ofisini kwake leo juu
ya urejeshwaji rasmi wa matangazo ya kituo cha Televisheni cha Tanga Televisheni
kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga. Matangazoyameanza Juni 12 , 2014 kituo kilipoanza kurusha
matangazo ya majaribio.
Matangazo hayo yanapatikana kupitia king’amuzi cha kampuni ya Startimes,
channel no 109 katika Mkoa wa Tanga. Kituo cha Tanga Televisheni kilikatisha matangazo
yake mnamo tarehe 12 Januari, 2013 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utangazaji
ambapo awali kiliendeshwa kwa mfumo wa analogia.
Kwa sasa kituo cha Tanga TV kinaonekana katika maeneo ya Wilaya za Tanga, Muheza,
Pangani, Mkinga na Pemba ambapo Uongozi wa
Halmashauri unafanya jitihada zaidi ili kuwafikia wakazi wote wa Wilaya za Tanga. Tanga
Televisheni ni kituo cha kwanza cha Halmashauri nchini kuingia katika mfumo wa
digitali.
Wito unatolewa kwa Wakazi
wa Tanga kukipenda na kutumia kituo hiki
kupata
taarifa mbalimbali za mkoa wa Tanga na kitaifa na pia katika kukuza
vipaji vyao
kupitia kazi za kitaaluma, michezo na pia kazi za sanaa.
Kulia ni Bw. Musa Labani, Mkuu wa Kituo cha Tanga Televisheni pamoja na Wanahabari kutoka Kituo hicho
Waandishi wa Habari wa Tanga wakati wa mkutano
0 comments: