Wanawake Wakikristo Nchini Watakiwa Kuimarika Kiroho kwa manufaa ya Taifa
1
Wanawake wenye imani ya Kikristo nchini
wametakiwa kuimarika kiroho ili kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa katika
maisha yao kwa manufaa ya Taifa.
Wito huo umetolewa na Serikali katika hotuba iliyosomwa
na Mhe. Mboni Mgaza, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Tanga kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mama Mkristo kutoka Kanisa la
Anglicana (UMAKI) Dayosisi ya Tanga unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya
Galanos Jijini Tanga. Kauli mbiu ya mkutano ni Mwanamke amka uangaze nuru yako
imekuzukia Isaya 60:1.
Pamoja ya mambo ya kiroho kujadiliwa , kutakuwepo na mada
mbalimbali zikiwemo; Athari ya Mabadiliko ya nchi, Ujasiriamali na Vikoba, ndoa
na Ukimwi na majadiliano mbalimbali. Jumla ya washiriki 315 wameshiriki kutoka Wilaya
mbalimbali.
Rev. Cecilia Kwikima , mshereheshaji wa Mkutano akitoa
utambulisho wa washiriki wa mkutano
Mwanaamani
Mtoo, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga akitoa utambulisho wa Uongozi wa Serikali
Sehemu ya washiriki wakionyesha hisia zao wakati wa
wimbo wa kuhamasisha kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
wanaotunzwa na kitengo cha Hospiece kinachomilikiwa na Kanisa la Anglicana
Dayosisi ya Tanga ulioimbwa na mtoto
Reonald Sembe (hayupo pichani) uitwao “Wazazi wangu wangekuwepo…….”
Mfano wa bidhaa ambazo zinatengenezwa na
akinamama hao ikikabidhiwa kwa Mhe. Mboni Mgaza ikiwa ni zawadi.
Gloria
Kiondo , Mshiriki kutoka Wilaya ya
Lushoto akitoa maelezo ya bidhaa wanazotenengeza
Bidhaa
nyingi zaidi kutoka kwa Washiriki wa Mkutano
Baadhi
ya washirikiwa mkutano
Picha ya pamoja ya Mhe. Mboni Mgaza na washiriki
wa mkutano
0 comments: