Serikali Mkoani Tanga yachukua Tahadhali Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola
Afisa Afya kutoka Hospitali ya Bombo Bw. Said Ibrahim
akifundisha kwa vitendo jinsi ya uvaaji wa mavazi na vifaa maalumu wakati wa
kutoka huduma ya kitabibu kwa mgonjwa wa Ebola . Aliyevaa mavazi maalumu ni Dr
Nakiete Mchomvu.
SERIKALI imetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa
mgonjwa yeyote mwenye dalili ya ugonjwa
wa Ebora ili aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi
kwa watu wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa hatari wa
Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma kwa
madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi kilichofanyika leo
katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga (Bombo).
Kikao hicho ni moja ya
jitihada ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa wa ugonjwa huo hatari ambao sasa umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya
Afrika. Vile vile ametoa wito kwa sekta
ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu zao pamoja katika kuhakikisha wanachi
wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa
dhidi ya jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika
Mkoa wa Tanga, Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Dr Asha Mahita amesema
kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili kutoa huduma
ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni pamoja na eneo la
Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga na kituo kingine kipo
Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua
tahadhali katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro mpaka wa Tanzania na Kenye na uwanja wa ndege
kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na kutambua msafiri mwenye
maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo
imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za jirani
na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya
ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya,
Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka Chama cha Watoa huduma
Binafsi za Afya Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo
la msingi iwapo Serikali na Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili
kudhibiti na kuzuia ebola kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake
hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa
yeyote mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika
nchi ya Tanzania. Historia inaonyesha
mwaka 2012 Mwezi wa Julai ulitokea
mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi
mwa Uganda eneo linaitwa Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari
unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virusi na
husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali inayoambatana na
kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na
ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha damu.
DSCO4681Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo akifungua
rasmi kikao hicho .Kulia ni Kaimu Mganga
Mkuu Mkoa waTanga Dr Asha. Mahita na Mtendaji Mkuu kutokaChama cha Watoa Huduma
binafsi za Afya Nchini, Dr. Samweli Ogillo.
Afisa Afya Mkoa wa Tanga Bw. Magoma akitoa maelezo juu ya ugonjwa wa Ebola
Wajumbe wa Kikao wakisikiliza kwa makini
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita
akizungumza na wajumbe muda mchache kabla ya Mgeni rasmi kufungua kikao rasmi.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo na kulia na Mtendaji
Mkuu Kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za Afya, Dr Samweli Ogillo
Mtendaji Mkuu kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za
Afya Dr Samweli Ogillo akitoa dhana ya ushirikiano baina ya sekta Binafsi na
Sekta ya Umma katika kuboresha huduma za afya. Kushoto ni Mganga Mkuu Mkoa wa
Tanga Dr Asha Mahita na Mkuu wa wilaya
ya Tanga Mhe. Halima Dendego.
Picha ya pamoja ya wajumbe na mgeni rasmi
0 comments: