Watumishi Wa Halmashauri Watakiwa Kuacha Kukaa Ofisini


Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Halima Dedengo akitoa ufafanuzi  juu ya stend mpya ya Mkoa wakati wa ziara ya siku mbili ya  Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Mhe. Chiku Gallawa kutembelea miradi ya maendeleo katika jiji la Tanga. 
 
Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kuacha kukaa ofisini na kupiga soga badala yake watoke waende kwa wananchi kuhimiza maendeleo pamoja na  kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na kuangalia namna gani ya kuzipatia ufumbuzi.
                                                                             
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati wa ziara yake ya siku mbili kwenye wilaya ya Tanga iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari wilaya ya Tanga.

Alisema kuwa kukaa ofisini kwa watumishi hao kumekuwa kukichangia kwa asilimia kubwa kurudisha nyuma kasi ya maendeleo kwenye maeneo yanayopaswa kuyasimamia kutokana na wao kushindwa kufahama namna aina ya changamoto zinazowakabili.


      “Sidhani kama ni sahihi kwa watumishi wa Halmashauri kuendelea kukaa ofisini,hii sio sawa sasa mnatakiwa mtoke mwende kwa wananchi mnaangalia wanakabiliwa na matatizo gani ili muweza kuyapatia ufumbuzi “Alisema Gallawa.


Aidha aliwataka watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanabadilika kwa kutambua kazi zao wanazofanya ili waweze kuchangia kasi ya maendeleo kwenye maeneo wanayokuwa wakiyaongoza.


Aliwataka kushirikiana na watendaji wa ngazi za chini ili waweze kuwasaidia wananchi waliopo kwenye maeneo wanayopaswa kusimamia ipasavyo kwa kuweka mipango mizuri itakayoleta matokea mazuri kwao.

Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa aliamua kuchukua uamuzi wa kufuta viwanja
12 vilivyotolewa kwenye eneo la stendi mpya ya mabasi kwa watu binafsi badala yake watafute mwekezaji mmoja ambayo atajenga jingo la ghorofa nne na kuwapangisha wafanyabishara.


Hata hivyo wakati mkuu huyo wa mkoa alipofanya ziara yake kwenye eneo la stendi hiyo kulitokea mvutano baina yake na Mstahiki wa Meya ya Jiji la Tanga Omari Guledi kutokana na mwekezaji mzawa kampuni ya mabasi ya Ratco alijitokeza kutaka kuwekeza lakini Halmashauri ilikataa.

Halmashauri hiyo ilimkataa mwekezaji huyo kutokana na kushindwa kuendana na mipango yao ambapo wao walitaka kujengwe jengo la ghorofa nne lakini yeye akata ajenge nyumba za kawaida jambo ambalo lilipigwa na uongozi wa Halmashauri. Stori na Picha na Osca Assenga- Tanga
 


Written by

0 comments: