Bonanza La Watumishi Tanga Lapamba Maadhimisho Ya Miaka 53 Ya Uhuru

Katika maadhimisho ya miaka 53 ya  Uhuru jana,Watumishi katika  Mkoa wa Tanga walisherehekea kwa  kushiriki katika michezo mbalimbali lengo likiwa ni kujenga umoja na ushirikano  baina ya watumishi wa Ras Tanga, Mashirika ya Umma na taasisi za Serikali. Pichani ni timu ya Ras Tanga wakichuana na timu ya Magereza 
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima (Alhaji) akifungua rasmi bonanza la michezo la watumishi lilifanyika jana wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika 
 
Bw. Chima ametoa rai kwa watumishi kupenda michezo na kuwa na kawaida ya kufanya mazoezi kwani husaidia kuchangamsha mwili na akili. Ametoa rai hiyo huku akisisitiza kuwa  ni vyema watumishi kutumia fursa kama hiyo katika kujenga mahusiano mazuri kazini ambayo huleta umoja na mshikamano katika kazi 
 Bonanza lilianza kwa mazoezi ya viungo 


 Timu ya Magereza wakichuana na timu ya Rs Tanga ( Hawapo pichani)  
  Timu ya Ras Tanga na Timu ya Netboli ya Queens wakichuana
 Timu ya Mikanjuni Vetenari wakichuana na Ras Tanga
 Baadhi ya washiriki katika bonanza
 Wachezaji wakichuana katika mchezo wa bao. Bao ni mchezo maarufu katika Mkoa wa Tanga


Written by

1 comment: