RHMT Tanga yajikita katika uboreshaji wa huduma za afya
Timu ya Uendeshaji wa
huduma za Afya katika Mkoa wa Tanga (RHMT) imeendelea kuhakikisha kuwa huduma
za Afya katika Vituo mbalimbali vya afya katika Mkoa wa Tanga zinakuwa na
mazingira mazuri ya kuviwezesha kutoa huduma bora.
Hayo yanathibitishwa na
usimamizi unaofanywa mara kwa mara na timu ya Usimamizi wa huduma za afya ya Mkoa. Lengo kuu ni kutaka kujua mazingira ya
kazi na changamoto zinazojitokeza katika vituo vya afya katika Mkoa wa Tanga na
hatimaye kuona ni jinsi gani mamlaka za Mkoa zinavyoweza kuboresha huduma.
Ikiwa kwenye usimamizi
shirikishi katika Wilaya ya Mkinga wiki iliyopita, timu ya Mkoa iliyokuwa na
wajumbe watano ambayo wajumbe wake ni Dr Clemence Marcel, Neema Shosho, Charles Kijazi
, Monica Laurent na Joyce Magembe iliweza kujionea hali halisi ya mazingira ya kazi katika
vituo mbalimbali vya afya na kubaini
kuwa ipo changamoto ya wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya (CHF).
Ilionekana pia kuwa ipo haja ya viongozi wa serikali na viongozi wakisiasa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamaisha
wananchi ili kujiunga na mfuko huu muhimu. Faida zinazotokana na Bima ya afya (CHF)
ni pamoja na faida ya tele kwa tele ambayo kituo cha afya hupatiwa kutokana na uchangiaji wa wananchi katika kituo husika.
Timu pia iliweza kupata fursa ya kutoa ushauri kwa ngazi mbalimbali za Wilaya
ili kusaidia upatikanaji wa madawa na
vifaa tiba kwa wakati.
Dr
Justice Munisi ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkinga akielezea mpango kazi
wa idara ya Afya katika Wilaya yake
wakati timu ya RHMT ilipofika ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya
usimamizi shirikishi katika Wilaya ya Tanga . Kulia ni timu ya usimamizi huduma za afya katika Wilaya ya Mkinga wakifuatilia kwa makini.
Dr
Amina S. Ally ambaye ni Mtabibu katika kituo cha afya cha Mayomboni akitoa taarifa ya utendaji kwa timu ya
utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo. Kulia ni Charles Kijazi, Neema Shosho (Katikati ) na Dr Clemence Marcel
Bi.
Pili Azizi (kushoto) ambaye ni Mtabibu Msaidizi katika kituo cha afya cha Moa akionyesha sehemu ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba kwa timu ya
utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo. kulia ni Dr Clemence Marcel na Charles Kijazi
Dr.Mohamed
Ally ambaye ni Mtabibu katika Kituo cha
afya cha Vyeru akifafanua jambo kwa timu ya
utendaji ya Mkoa wakati timu hiyo ilipotembelea kituoni hapo
0 comments: