Mahakama Tanga Yazindua Bodi Mpya Ya Parole
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula Said
Magalula amewataka wajumbe wa Bodi ya Paroli Mkoa kutenda kazi kwa kufuata kanuni na taratibu
zilizowekwa ili kutenda haki na kuepuka ushawishi wa namna yeyote katika
kupokea na kuomba rushwa.
Hayo yamesemwa mapema siku ya alhamisi ya machi 12 mwaka huu wakati wa uzindua rasmi Bodi ya Parole Mkoa tukio lililofanyika katika ofisi za
Magereza Mkoa.
Lengo la Bodi hii ni kuwajadili
wafungwa wenye sifa za kuweza kuachiliwa
huru baada ya kutimiza vigezo ambavyo vimeainishwa kwenye sheria namba 25 ya Paroli ya mwaka 1994 na kufanyiwa
mabadiliko mwaka 2002.
Sheria husika imeweza
kuanisha ni aina gani ya makosa ambayo mfungwa anaweza kupata fursa ya kuingia
kwenye mpango wa Paroli . Pamoja na makosa hayo mfungwa hawezi kuingizwa kwenye
utaratibu wa Paroli endapo amepatikana na kosa la unyanyanyi wa siraha, madawa
ya kulevya, kulawiti, kubaka na mauaji ya kukusudia.
Akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa sheria ya parole tangu utekelezaji wake mwaka 2003, Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Tanga Kamishina Agustino Mboje amesema tayari wafungwa 331
wameshaachiliwa huru kwa utaratibu wa parole, wafungwa 305 wamemaliza vifungo
vyao salama na wafungwa 26 bado wanaendelea na vifungo vyao kwa utaratibu huu.
Licha ya kuwepo na mpango
huu wa kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani lakini bado wafungwa wengi
wameshindwa kunufaika na utaratibu wa Paroli kutokana na kutotimiza masharti ya
parole.
Sababu kubwa ni ukosefu wa
nakala za hukumu kwa wakati na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wanajamii kuhusu sheria hii na hivyo
kupelekea maafisa wa Paroli kuwa na
ugumu wa kupata taarifa muhimu zinazowahusu wafungwa wananotarajiwa kunufaika
na mpango huu.
Maafisa wa Magereza wakimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Mhe. Magalula Said Magalula
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akisaini kitabu cha wageni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kam. Augostino Mboje
akitoa taarifa ya utekelezaji wa sheria ya Parole katika Mkoa wa Tanga
Baadhi ya wajumbe na Maafisa wa magereza wakati wa
uzinduzi
0 comments: