BREAKING NEWS
Breaking
news……………………………..!
AJALI MBAYA YASABABISHA VIFO
VYA WAANDISHI WA HABARI NA AFISA UHAMIAJI WILAYANI HANDENI
Ajali hiyo imetokea katika
kijiji cha Misima katika barabara ya Handeni Korogwe ikihusisha gari la
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni. Gari hiyo ilkuwa katika msafara wa ziara
ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Muhingo Rweyemamu wakielekea katika shughuli
ya upandaji miti.
Watu watatu wamefariki dunia
wakiwemo Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni Bi. Mariam Hassani, Mwandishi wa
Habari Bw. Hamis Bwanga aliyekuwa akiripotia gazeti la Uhuru na Radio Abood na
mwandishi wa Habari Bw. Hussen Semdoe aliyekuwa akiripotia gazeti la Mwananchi.
Aidha wamepatikana
majeruhi wannne ambao ni watumishi wa
Halmashauri ya Handeni. Juhudi za
kuwakimbiza majeruhi katika hospitali ya KCMC (Kilimanjaro) zimekamilika na
taratibu za mazishi zinaendelea .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatoa pole kwa wafiwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Ofisi ya Uhamiaji ,Tasinia ya Habari na
wananchi kwa ujumla .
Tutaendelea kupashana
yanayojili.
poleni sana wana tanga
ReplyDeleteahsante sana
Delete