Wakazi wa Mkoa wa Tanga waonyesha Mshikamano katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2013.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe .Chiku
Gallawa akiupokea Mwenge wa Uhuru ambao umetokea Mkoa wa Mjini Magharibi kwa
lengo la Kukimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga. Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka huu, zimebeba ujumbe usemao: “Watanzania
ni Wamoja” wenye kauli mbiu “ Tusigawanywe kwa misingi ya Tofauti zetu za
Dini, Itikadi, Rangi na Rasilimali” Lengo la Ujumbe na Kauli Mbiu hii ni
kutoa msisitizo kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kuimarisha Umoja na Amani katika jamii .
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa Bw. Juma Ali Simai akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa
Barabara za viwandani eneo la Gofu Viwandani. Mradi huo unategemea kunufaisha
wawekezaji wengi na wananchi kwa ujumla.
Wakazi wa Wilaya ya Tanga
wakifurahia ufunguzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngamiani. Wakazi hao wameweza
kudhihirisha kuwa wao ni wamoja na maendeleo ya Tanga ni ya wote . Mradi huo ni
miongoni mwa miradi mbalimbali iliyofunguliwa na iliyozinduliwa wakati wa kukimbiza
mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Tanga ikiwemo uzinduzi wa jengo la Wazazi
katika Zahanati ya Duga, Mradi wa kusambaza Umeme katika eneo la Sahare,kituo cha kukusanya maziwa Kichangani,
ufunguzi wa mradii wa Maabara katika shule ya secondary ya Wasichana St
Christina, uzinduzi wa vikoba na uzinduzi wa
Club ya Wapinga Rushwa . Miradi yote wilayani Tanga imegharimu kiasi cha
fedha za kitanzania 8,580,270,458.
Vijana wa halaiki wakiyapamba mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika
Wilaya ya Tanga. Wilaya pia ilijiandaa
vyema kwa burudani mbalimbali na kufanikisha sherehe za mapokezzi
kufana.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh Halima
Dendegu akitoa neno la shukurani kwa wakazi wa Tanga na vijana wakimbiza Mwenge
mara tu baada ya risala ya Utii kwa Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments: